MAGAZETI ya Leo Jumapili 25 May 2025

MAGAZETI ya Leo Jumapili 25 May 2025 Klabu ya Yanga imetangaza kuachana rasmi na aliyekuwa kiungo mshambuliaji wake, Stephane Aziz Ki ambaye amesajili na Wydad Athletic ya Morocco. Kiungo huyo anaondoka Young Africans akiwa ameacha historia kubwa baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mitatu akitokea ASEC Mimosas ya Ivory Coast. Aziz Ki alicheza mechi yake ya mwisho Yanga na kupewa heshima ya kuwa nahodha mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la FA na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Rais Mstaafu Thabo Mbeki Aitaka Afrika Kuwa na Ajenda Yake

Rais wa Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo akizungumza katika Mkutano wa Kibiashara wa Ngazi ya Juu uliodhaminiwa na AngloGlod Ashanti uliofanyika jijini Dar es Salaam. Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Thabo Mbeki, ameitaka jumuiya ya wafanyabiashara barani Afrika kuweka ajenda yenye mwelekeo wa pamoja na malengo makubwa kuelekea Urais wa G20 wa Afrika Kusini mwaka 2025. Akizungumza katika Mkutano wa Kibiashara wa Ngazi ya Juu uliofanyika jijini Dar es Salaam, Bw. Mbeki alisisitiza umuhimu wa kushughulikia masuala muhimu kama mshikamano, usawa na maendeleo endelevu, kwa kuzingatia zaidi maendeleo ya bara la Afrika. Mbunge wa Bumbuli Januari Makamba akisalimiana na Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki wakati wa mjadala wa pamoja na wadau mbalimbali kuhusu mustakabali wa Afrika katika hoteli ya Rotana uliofadhiliwa na AngloGold Ashanti. Mkutano ujao wa G20, ambao utafanyika Afrika Kusini, unalenga kukabiliana na changamoto zinazohusiana kimataifa ikiwa ni pamoja na umaskini, ukosefu wa ajira, usawa wa kijamii, mabadiliko ya tabianchi, usalama wa chakula na nishati, miongoni mwa mengine. Akizungumza katika mkutano huo — ulioratibiwa kwa pamoja na Taasisi ya Thabo Mbeki na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, na kudhaminiwa na AngloGold Ashanti — Bw. Mbeki alibainisha kuwa, licha ya juhudi mbalimbali zilizofanyika alipokuwa madarakani, sasa ni wakati wa sekta binafsi Afrika kuongoza katika kuunda ajenda ya kiuchumi ya bara hili kimataifa. Simon Shayo, Makamu wa Rais wa Masuala ya Uendelevu ( Afrika) katika kampuni ya AngloGold Ashanti akiongea mbele ya hadhira akiwemo Rais mstaafu wa Afrika Kusini Mr Thabo Mbeki katika kujadili masuala ya Afrika katika moja za matukio ya Siku ya Afrika 2025 katika hoteli ya Rotana jijini Dar es Salaam. Mkutano huo, uliofanyika katika Hoteli ya Rotana, Dar es Salaam kama sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 15 ya Mhadhara wa Siku ya Afrika, uliwakutanisha viongozi wa kibiashara, wawakilishi wa sekta binafsi, wasomi na wanadiplomasia. Bw. Mbeki aliwasihi washiriki kuunda ajenda ya kiuchumi ya pamoja ya Afrika kwa ajili ya jukwaa la kimataifa. “Lazima tuwe na mpangilio na kuzungumza kwa sauti moja kuhusu masuala ya msingi.” , alisema huku akiwakumbusha kushindwa kwa Mpango wa Utekelezaji wa Afrika (Africa Action Plan) katika miaka ya nyuma, akitoa wito wa kuandaa mapendekezo ya sera yatakayoongozwa na Waafrika. “Tulikuwa na juhudi kadhaa katika mikutano ya G8 kushinikiza ajenda ya maendeleo ya Afrika kwa kutumia rasilimali zetu wenyewe. Sasa, kwa kuwa Umoja wa Afrika ni mwanachama wa G20, tunapaswa kutumia fursa hii kusukuma mbele ajenda yetu,” aliongeza Bw. Mbeki. Mkutano huo wa G20 unaotarajiwa kufanyika Johannesburg mwezi Novemba 2025, utakuwa wa kwanza kufanyika katika ardhi ya Afrika — jukwaa muhimu la kusukuma mbele maslahi ya bara hili. Pamoja na Umoja wa Afrika, wanachama wa G20 ni pamoja na Argentina, Australia, Brazil, Canada, China, Ufaransa, Ujerumani, India, Indonesia, Italia, Japan, Korea Kusini, Mexico, Urusi, Saudi Arabia, Afrika Kusini, Uturuki, Uingereza, Marekani, na Umoja wa Ulaya. Wakati wa mkutano huo, washiriki walihimiza mataifa ya Afrika kujielekeza katika kutetea maslahi yao na kuweka njia ya maendeleo inayotegemea rasilimali zao, ikiwa ni pamoja na madini. Mchumi mashuhuri Profesa Samwel Wangwe alisisitiza hitaji kwa mataifa ya Afrika kurejea katika misingi ya kujitegemea na kutathmini upya nafasi ya Umoja wa Afrika. Alipendekeza pia umoja wa Afrika, kuanzishwa kwa sarafu ya pamoja, ulinzi wa rasilimali asilia, uwekezaji katika ujuzi wa ubunifu wa kibiashara, na kuweka mazingira rafiki kwa ukuaji wa uchumi kupitia ushirikiano thabiti kati ya sekta ya umma na binafsi. Mkutano huo uliopewa kaulimbiu: “Kujenga Mwelekeo wa Pamoja kwa Ajili ya Mkutano wa Urais wa G20 wa Afrika Kusini: Kufufua Uamsho wa Afrika’, ulilenga kuandaa msimamo wa pamoja wa wafanyabiashara wa Afrika kwa majadiliano yajayo ya G20. Akifungua kikao hicho, Simon Shayo, Makamu wa Rais wa AngloGold Ashanti, alitoa wito wa mabadiliko katika namna sekta binafsi inavyoshiriki kwenye maendeleo. “Lazima tuwe zaidi ya wadau wa kiuchumi lazima tuwe wasanifu wa mustakabali wa Afrika,” alisema Shayo, akirejelea mchango wa kampuni yao wa zaidi ya miaka 25 katika sekta ya madini nchini Tanzania. Lukhanyo Neer, Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Taasisi ya Thabo Mbeki, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano unaovuka mipaka ya kitaifa na ya kibiashara. “Tunahitaji sauti moja ya Afrika katika majukwaa ya kiuchumi ya kimataifa,” alisema. Balozi John Ulanga wa Tanzania aligusia changamoto kubwa, akisema Afrika inapata theluthi moja tu ya uwekezaji wa miundombinu unaohitajika. Alipendekeza kuwekeza kwenye miradi ya pamoja ya miundombinu ya bara kama vile mradi wa Cape to Cairo, pamoja na kuweka mifumo ya kusaidia biashara kwa vitendo. “Utekelezaji lazima uongozwe na wakuu wa nchi lakini ujikite katika uhalisia wa Afrika,” alisema Ulanga. Balozi Ami Mpungwe alitoa wito wa kufikiria upya mtazamo wa maendeleo ya Afrika. “Rasilimali pekee si suluhisho — ni msingi tu,” alieleza. Akisisitiza umuhimu wa uwekezaji katika teknolojia, mitaji, na vipaji, alitaja uwekezaji wa Afrika Kusini nchini Tanzania kama mfano bora wa mafanikio ya ndani ya bara. Majadiliano katika mkutano huo pia yaligusia sekta muhimu kama vile nishati, biashara, na kilimo. Washiriki walihimiza kubadili mtazamo kutoka kuuza mazao ghafi hadi usindikaji wenye thamani zaidi, wakitaja mazao kama korosho kuwa na fursa kubwa ya kiuchumi. Uwezeshaji wa vijana na ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi pia ulitambuliwa kama nguzo kuu za ukuaji wa uchumi. Katika hotuba ya kufunga mkutano, Emily Kariuki kutoka Taasisi ya Mbeki Ndlela alikumbusha urithi wa Mwalimu Julius Nyerere. “Tunaposhirikiana kama Afrika, hatuzuiliki hata katika majukwaa magumu ya kimataifa,” alisema, akiwahimiza washiriki kudumisha ari hiyo. Mkutano huo ulimalizika kwa ahadi thabiti ya kujenga jukwaa la pamoja na la kimkakati la wafanyabiashara wa Afrika kwa ajili ya kushiriki katika G20. Wakati wa majadiliano, AngloGold Ashanti ilithibitisha tena dhamira yake ya kuendelea kusaidia majukwaa kama haya, ikiahidi kuendelea kuwa kichocheo cha maendeleo jumuishi na endelevu barani Afrika.

GSM Group Yadhamini Mbio za Marathon za Siku ya Afrika 2025

GSM Group imedhamini mbio za marathon za Siku ya Afrika 2025, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kuenzi Umoja wa Afrika na kuimarisha mshikamano wa bara zima. Tukio hilo kubwa limefanyika leo tarehe 25 Mei 2025, likihusisha mbio za umbali wa 5KM, 10KM na 21KM, na limevuta washiriki zaidi ya 1,000 wakiwemo maafisa wa serikali, wanadiplomasia, wananchi, pamoja na wanariadha maarufu wa Tanzania. Mbio hizi ni sehemu ya maadhimisho ya kila mwaka ya Siku ya Afrika, siku inayoadhimisha kuanzishwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) mwaka 1963, ambao sasa ni Umoja wa Afrika (AU). Kaulimbiu ya mwaka huu inalenga kuimarisha mshikamano wa kikanda, biashara huru, na maendeleo jumuishi kupitia mkataba wa AfCFTA. Kupitia udhamini huu, GSM Group imetoa huduma ya maji safi ya kunywa kupitia bidhaa yake ya GSM Pure Drinking Water kwa washiriki wote wa mbio hizo. Udhamini huu unaonyesha dhamira ya kampuni hiyo ya kusaidia shughuli za kijamii, kiafya na kiutamaduni ambazo zina mchango chanya kwa jamii ya Kiafrika. Kwa kuongezea, GSM Group pia ilishiriki katika shughuli nyingine za kuadhimisha Siku ya Afrika, zikiwemo: • Mei 17, 2025 – Mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu kati ya timu ya Nje Sports na timu ya Jumuiya ya Kidiplomasia Afrika. • Mei 23, 2025 – Gala Dinner ya kuwakutanisha wanadiplomasia, viongozi wa serikali na wadau wa sekta binafsi katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam. Mgeni rasmi wa Gala dinner hii alikuwa Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Mh. Thabo Mbeki. Kwa ushiriki wake katika maadhimisho haya, GSM Group inathibitisha nafasi yake kama mshirika wa maendeleo ya kijamii, mdau mzuri wa michezo na muwekezaji wa juhudi zinazojenga Afrika bora ya baadae.

Waziri Mkuu Anadi Vivutio Vya Utalii, Uwekezaji

Ni katika siku ya Tanzania kwenye maonesho ya Osaka World EXPO 2025 Asema mauazo ya bidhaa za Tanzania Japan yafikia sh bilioni 37 Asisitiza Tanzania ni mahali salama kwa uwekezaji WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema ushirikiano wa Tanzania na Japan umezidi kukua katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia umezidi kuimarika siku hadi siku, ambapo mauzo ya biashara kati ya nchi hizo yameongezeka kutoka dola za Marekani bilioni saba mwaka 2023 hadi bilioni 37 kwa mwaka 2024. Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumapili, Mei 25, 2025) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa maadhimisho ya Siku ya Tanzania kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Osaka (World Expo Osaka 2025) yanayoendelea nchini Japan. Amesema Wajapan wanapenda sana bidhaa kutoka Tanzania zikiwemo za kilimo kama chai, kahawa, ufuta, tumbaku, tingatinga, vinyago, katani, viungo kama karafuu pamoja na madini mbalimbali yanayopatikana nchini. Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa Japan na duniani kote waje kuwekeza katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya elimu, afya, miundombinu, nishati, kilimo, utalii kwani Tanzania imeweka mazingitra mazuri ya uwekezaji na pia ina amani na utulivu. “…Tanzania licha ya kuwa na fursa nyingi za uwekezaji ikiwemo ardhi yenye rutuba, amani na mazingira tulivu, pia ni kitovu cha biashara katika Ukanda wa Afrika Mashariki, Kusini na Kati kwa kuwa inapakana na nchi saba ambazo ni Uganda, Rwanda, Burundi, Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Zambia, Malawi na Msumbuji hivyo kuwawezesha wawekezaji kupata masoko ya uhakika katika mataifa hayo.” Waziri Mkuu amesema Serikali ipo katika mchakato wa kuvifanyia maboresho viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere maarufu sabasaba ili viwe na hadhi ya kimataifa na kuwezesha kufanyika mikutano na maonesho ya biashara ya kikanda na kimataifa. Monesho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanziba wakiwemo Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi mbalimbali. Maonesho hayo yalianza tangu Aprili 13, 2025 na yanatarajia kumalizika Oktoba 13, 2025, hii ni mara ya pili kwa Japan (Osaka) kuwa mwenyeji wa maonesho hayo ya kimataifa, ambapo mara ya mwisho yalifanyika 1970 (EXPO 1970). Kesho (Jumatatu, Mei 26, 2026), Mheshimiwa Majaliwa anatarajiwa kushiriki katika kongamano la biashara, uwekezaji na utalii ambalo litahusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Japan. Pia, Waziri Mkuu atashiriki katika Mikutano ya Uwili na viongozi wa Serikali ya Japan, mashirika ya maendeleo na watendaji wakuu wa makampuni mbalimbali kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.

GATES OF OLYMPIA – MLANGO WA USHINDI UMESHAFUNGULIWA…

Jukwaa la mabingwa wa michezo ya kubahatisha Tanzania, linakuletea mchezo mpya wa kisasa na wa kuvutia: GATES OF OLYMPIA. Ukiwa umejengwa kwa hadithi ya Kigiriki, mchezo huu unakuweka uso kwa uso na mungu wa radi Zeus, huku akikusambazia zawadi, spins na multipliers za ajabu! KWA NINI UCHEZE GATES OF OLYMPIA KWENYE MERIDIANBET? Ushindi Mkubwa, Bila Kisingizio: Mchezo huu una odds kubwa, spins za bure za mara kwa mara, na multipliers hadi x500 – yaani dau dogo linaweza kukuletea mamilioni ya papo kwa papo! Ubunifu wa Kisasa: Graphics kali, animation za kuvutia na sauti zenye mvuto – Gates of Olympia ni zaidi ya slot, ni safari ya kipekee ya ushindi. Bonasi Zilizopangwa kwa Ajili Yako: Wateja wote wa Meridianbet wana nafasi ya kupata bonasi maalum wakicheza Gates of Olympia. Cheza Kiganjani Mwako: Kupitia App ya Meridianbet au tovuti yetu rahisi kutumia, una uhuru wa kucheza popote na muda wowote! PROMOSHENI MAALUM: Kwa kila mchezaji mpya anayejisajili na kucheza Gates of Olympia: Unapata Free Spins moja kwa moja! Unajiingiza kwenye droo ya kila wiki kushinda zawadi maalum kama bonasi za pesa taslimu. Usikubali Hadithi za Wengine – Jiandikie Ya Kwako! Huu ndio wakati wa kujaribu bahati yako kwa mchezo wa kiwango cha kimataifa. Tembelea www.meridianbet.co.tz sasa au pakua App ya Meridianbet, uanze safari yako ya ushindi na Gates of Olympia! MERIDIANBET – TULIPO, USHINDI HAUISHI! Tovuti: www.meridianbet.co.tz Huduma kwa Wateja: IPO App: Pakua kwenye Play Store au App Store  NB: Jisajili na Meridianbet na cheza michezo ya kasino ya mtandaoni upate ushindi kirahisi, Pia ongeza maokoto yako kwa kubashiri michezo mbalimbali yenye ODDS KUBWA. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz   The post GATES OF OLYMPIA – MLANGO WA USHINDI UMESHAFUNGULIWA… appeared first on Soka La Bongo.

MAGAZETI ya Leo Jumapili 25 May 2025

Rais Mstaafu Thabo Mbeki Aitaka Afrika Kuwa na Ajenda Yake

GSM Group Yadhamini Mbio za Marathon za Siku ya Afrika 2025

Waziri Mkuu Anadi Vivutio Vya Utalii, Uwekezaji

GATES OF OLYMPIA – MLANGO WA USHINDI UMESHAFUNGULIWA…

Lastest News

Don't miss daily news

© Image Copyrights Title

Ufanisi wa TCAA Wapongezwa na Msajili wa Hazina

  • 11 Apr 2025
  • 8
© Image Copyrights Title

Tundu Lissu Asomewa Shitaka la Uhaini Mahakama ya Kisutu

  • 10 Apr 2025
  • 15
© Image Copyrights Title

Oparesheni ya TAWA Yaua Fisi 43 Itilima, Bariadi na Maswa

  • 10 Apr 2025
  • 11
© Image Copyrights Title

Bolt Yazindua Rasmi Huduma Zake Katika Mji wa Kahama

  • 10 Apr 2025
  • 10
© Image Copyrights Title

Shaka Ssali Kufanyiwa Heshima za Mwisho Leo Marekani

  • 10 Apr 2025
  • 10
Read more News

Burudani

Don't miss daily news

© Image Copyrights Title

Chris Brown ashitakiwa kwa kumshambulia mtu kwenye klabu ya Usiku

Lorem ipsum dosectetur adipisicing elit, sed do.Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur Nulla fringilla purus at leo dignissim congue. Mauris elementum accumsan leo vel tempor.

  • 38
Read all News
© Image Copyrights Title

Chris Brown ashitakiwa kwa kumshambulia mtu kwenye klabu ya Usiku

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 38
© Image Copyrights Title

D Voice Atarajia Kuachia Ep yake Mpya

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 43
© Image Copyrights Title

Bobby Shmurda Asitisha Tour Yake, Auza Tiketi 10 Tu Kila Mji.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 35
© Image Copyrights Title

Wasanii Wanaowania Tuzo Za BET 2025.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 24
© Image Copyrights Title

Diamond Mfalme Wa Youtube Africa.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 43
© Image Copyrights Title

Rihanna Na Asap Rocky Watarajia Kupata Mtoto Wa 3.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 41
© Image Copyrights Title

Yammi Aacha Na Label Ya Nandy ‘The African Princess’.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 47
© Image Copyrights Title

Mtuhumiwa Aliyemuibia Kim Kardashian Afariki Dunia Kabla Ya Kesi Kuanza.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 29
© Image Copyrights Title

Mtuhumiwa Aliyemuibia Kim Kardashian Afariki Dunia Kabla Ya Kesi Kuanza.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 21
© Image Copyrights Title

Jux Ashinda Tuzo Ya Msanii Bora Afrika Mashariki Kwenye The Headies Nigeria.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 33

Michezo

Don't miss daily news

© Image Copyrights Title

GATES OF OLYMPIA – MLANGO WA USHINDI UMESHAFUNGULIWA…

Lorem ipsum dosectetur adipisicing elit, sed do.Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur Nulla fringilla purus at leo dignissim congue. Mauris elementum accumsan leo vel tempor.

  • 38
Read all News
© Image Copyrights Title

GATES OF OLYMPIA – MLANGO WA USHINDI UMESHAFUNGULIWA…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 38
© Image Copyrights Title

CHUKUA CHAKO MAPEMA LEO…ODDS ZA USHINDI HIZI HAPA…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 42
© Image Copyrights Title

MERIDIANBET YAPIGA HATUA KUBWA KATIKA ULINZI WA MAZINGIRA

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 39
© Image Copyrights Title

ODDS KUBWA ZA KUKUPATIA MSHIKO ZIPO MERIDIANBET…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 40
© Image Copyrights Title

WAKATI DR MWINYI AKIHAIDI MIL 260….HAYA HAPA MAMBO 5 YA KUIBEBA SIMBA KESHO…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 44
© Image Copyrights Title

AFRIKA KUSINI USO KWA USO NA TAIFA STAR….NGOMA KUCHEZWA UGENINI…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 27
© Image Copyrights Title

BAADA YA AZIZ KI KUBEBWA NA WAARABU….PACOME AJIANDAE KWA HAYA NDANI YA YANGA….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 39
© Image Copyrights Title

KAPOMBE:- TUTAKACHOWAFANYA HAWATAAMINI KAMA WAKO KWA MKAPA 😎😎😎….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 33
© Image Copyrights Title

20 IMPERIAL CROWN HII HAPA CASINO YA UHAKIKA YA KUTOBOA KIMAISHA…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 3
© Image Copyrights Title

FUNGUA MILANGO YA UTUKUFU NA GATES OF OLIMPIA – SASA KATIKA MERIDIANBET! 👑

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 3
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook