
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekamata jumla ya magari 15 kwa kosa la kubandika namba za usajili bandia “SSH 2530”, kinyume cha sheria za usalama barabarani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Septemba 04, 2025, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro, alisema kitendo hicho ni uvunjifu wa sheria na kinaadhibiwa kwa mujibu wa kifungu cha 13(i) cha sheria ya usalama barabarani.
“Kujibandikia namba hizo ni kinyume cha sheria za usajili. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote waliokamatwa na magari yao yamehifadhiwa kama vielelezo,” alisema Kamanda Muliro.
Jeshi la Polisi limewataka wananchi kufuata taratibu sahihi za usajili wa vyombo vya moto na kuacha kutumia namba bandia zinazoweza kuhusishwa na matukio ya uhalifu.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!