Muuguzi wa India asubiri kunyongwa Julai 16

Nimisha Priya Na mwandishi wetu, Elvan Stambuli Nimisha Priya alihukumiwa kifo kwa mauaji ya mwanamume mmoja ambaye alikuwa mshirika wake wa zamani wa kibiashara, Talal Abdo Mahdi – ambaye mwili wake uliokatwakatwa uligunduliwa kwenye tanki la maji mnamo 2017. Njia pekee ya kumuokoa muuguzi huyo ni kama familia ya Mahdi itamsamehe. Ndugu na wafuasi wake wametoa $1m (£735,000) kama diyah, au pesa ya damu, ili kulipwa kwa familia ya Mahdi. “Bado tunasubiri msamaha wao au matakwa mengine,” mjumbe wa shirika linalomtetea aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza – BBC. “Tarehe ya kunyongwa ( Julai 16 mwaka huu) imewasilishwa na mkurugenzi mkuu wa mashtaka kwa mamlaka ya jela. Bado tunajaribu kumwokoa. Lakini hatimaye familia inabidi ikubali kumsamehe,” Babu John, mwanaharakati wa masuala ya kijamii na mjumbe wa shirikamoja linalopigania kumuokoa nesi huyo alisema. Afisa katika wizara ya mambo ya nje ya India aliiambia BBC kwamba bado wanajaribu kuthibitisha maelezo hayo. Nimisha Priya alikuwa ameondoka katika jimbo la kusini mwa India la Kerala kwenda Yemen mwaka 2008 kufanya kazi ya uuguzi. Alikamatwa mwaka wa 2017 baada ya mwili wa Mahdi kugunduliwa. Msichana huyo mwenye umri wa miaka 34 kwa sasa amefungwa katika jela kuu ya Sanaa katika mji mkuu wa Yemen. Alishtakiwa kwa kumuua Mahdi kwa kumpa “kiwango cha juu cha dawa za kumtuliza” na kudaiwa kuukatakata mwili wake baada ya kufariki dunia. Hata hivyo, Nimisha alikanusha madai hayo. Mahakamani, wakili wake alidai kwamba Mahdi alimtesa kimwili, akampokonya pesa zake zote, akamnyang’anya pasipoti yake ya kusafiria na hata kumtishia kwa bunduki. Muuguzi huyo alisema alijaribu kumpa dawa ya ganzi Mahdi ili tu kuchukua pasipoti yake kutoka kwake, lakini dozi iliongezeka kwa bahati mbaya. Mnamo 2020, mahakama ya eneo hilo ilimhukumu kifo. Familia yake ilipinga uamuzi huo katika Mahakama ya Juu ya Yemen, lakini rufaa yao ilikataliwa mwaka wa 2023. Mapema Januari mwaka huu, Mahdi al-Mashat, rais wa Baraza Kuu la Wahouthi, aliidhinisha kunyongwa kwake. Mfumo wa mahakama wa Kiislamu wa Yemen, unaojulikana kama Sharia, unampa matumaini ya mwisho – kupata msamaha kutoka kwa familia ya mwathirika kwa kulipa pesa za damu.

China Yatoa Onyo Kwa Marekani Kuhusu Ushuru Mpya – Yaapa Kulipiza Kisasi

Serikali ya China imetoa onyo kali kwa utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump, kuhusu mpango wa kurejesha ushuru wa juu kwa bidhaa kutoka China kuanzia Agosti 1, ikisema kuwa hatua hiyo inaweza kuchochea mvutano mpya wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili makubwa kiuchumi duniani. Kupitia makala maalum iliyochapishwa na gazeti la serikali la People’s Daily, chini ya jina la kalamu “Zhong Sheng” – linaloashiria msimamo rasmi wa serikali ya China katika masuala ya kidiplomasia – Beijing imeonya kuwa haitakubali kushambuliwa kiuchumi bila kujibu. “China haitaacha mashambulizi ya kiuchumi dhidi yake yakiendelea bila hatua. Nchi yoyote itakayoshirikiana na Marekani katika kutusukuma nje ya minyororo ya usambazaji kimataifa, itakabiliwa na hatua za kulipiza kisasi.” China pia imesema itachukua hatua dhidi ya nchi nyingine zitakazoshiriki katika mikakati ya kuiondoa kwenye mfumo wa usambazaji wa kimataifa, hali inayoashiria upanuaji wa mzozo huu kuwa wa pande nyingi. Haya yanajiri licha ya makubaliano ya awali ya kibiashara yaliyofikiwa kati ya Marekani na China mwezi Juni 2025, ambayo yalilenga kupunguza mvutano uliodumu kwa miaka kadhaa. Hata hivyo, masuala muhimu kama ushuru wa upande mmoja, ulinzi wa haki miliki, na upatikanaji wa masoko bado hayajapatiwa suluhisho la kudumu. Rais Trump, kwa upande wake, alitangaza Jumatatu kuwa iwapo hakuna makubaliano mapya yatakayofikiwa kufikia Agosti 12, ushuru mpya utaanza kutumika rasmi Agosti 1. NAIBU WAZIRI MKUU BITEKO APASUA UKWELI – “KAWAIDA KUGAWANYIKA WAKATI wa UCHAGUZI -HATUWEZI KUFANANA”

KUHUSU ISHU YA AZIZ KI KUTAKIWA KUTEMWA WYDAD…..YANGA WAWAPA JIBU HILI WAARABU….

BAADA ya kucheza dakika 11 kwenye mechi mbili za Kombe la Dunia la Klabu dhidi ya Manchester City na Juventus, kiungo mshambuliaji wa Wydad, Stephane Aziz KI huenda asiwe sehemu ya kikosi hicho msimu ujao huku ikielezwa ili abaki kuna ishu anaisikilizia. Wydad ilicheza mechi tatu za michuano hiyo na kuondolewa hatua ya makundi bila ushindi ikianza na kichapo cha mabao 2-0 kutoka Man City ambapo Aziz KI alicheza kwa dakika saba, Juventus iliwachapa 4-1 Aziz KI akicheza dakika nne na ililala 2-1 dhidi ya Al Ain huku Aziz KI akiwa hakucheza kabisa mchezo huo wa mwisho. Mchango wake ndani ya klabu hiyo bado haujaonekana kwa kiwango kilichotarajiwa huku kwenye michuano ya Kombe la Dunia la Klabu akitanguliwa na Thembinkosi Lorch na Nordin Amrabat ambao wanacheza nafasi moja uwanjani. Lorch ambaye alicheza mechi zote tatu za Kombe la Dunia la Klabu akifunga bao moja, ndiye anayetajwa kushikilia hatma ya Aziz KI kwani Msauzi huyo anacheza hapo kwa mkopo akitokea Mamelodi Sundowns. Mkataba huo wa mkopo unamalizika Julai 31, 2025 huku kukiwa na ripoti kwamba Wydad imeridhishwa na uwezo wake, hivyo inatak kumsajili moja kwa moja. Kwa mujibu wa jarida la Kiarabu la Al-Botola, Aziz KI anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wa kigeni wanaoweza kuachwa na klabu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu mpya. Hii ni kutokana na shinikizo la kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni hadi watano ili kutokukiuka kanuni za Ligi Kuu ya Morocco (Botola Pro 1), wakati sasa Wydad wana jumla ya wachezaji 11 wa kigeni, hivyo kocha Mohamed Benhachem ametakiwa kuwasilisha majina ya wachezaji wa kupunguza ili wabaki watano. Ikiwa Wydad watakamilisha usajili wa Lorch kama inavyodaiwa, basi nafasi ya Aziz KI itazidi kuwa finyu, hali inayoweza kumfanya aondoke labuni hapo mapema kuliko ilivyotarajiwa. “Usajili wa Aziz KI una vificho vingi hadi sasa ukiniuliza alisaini mkataba wa muda gani siwezi kukupa jibu kwani haijajulikana kutokana na Wydad kushindwa kuweka wazi tofauti na Mwalimu (Selemani) ilivyokuwa, lakini ninachofahamu ni kwamba kocha hajaridhishwa na uwezo wa kiungo huyo anaweza akaondoshwa kikosini,” kilisema chanzo cha taarifa hiyo. “Wakati baadhi ya vyanzo vikizungumza nyota huyo alisajiliwa kwa mkopo akitokea Yanga kukiwa na kipengele cha kumnunua na kuna vyombo vingine vinaripoti alisaini mkataba wa miaka mitatu, hivyo hii ni shida.” Wakati ikielezwa hivyo, kwa mujibu wa Transfermarkt – tovuti inayojihusisha na soka ikiwemo usajili wa wachezaji, Aziz KI alisaini mkataba wa miaka miwili Wydad unaomalizika Juni 2027. Kuhusu suala la Mtanzania Mwalimu, chanzo kilidai huenda akarudishwa timu ya vijana moja kwa moja kwa ajili ya kuendelea kukuza uwezo tofauti na awali ilivyokuwa ambapo alikuwa anapata nafasi ya kucheza timu ya wakubwa. Awali, ilielezwa Aziz KI aliyeitumikia Yanga kwa misimu mitatu tangu Julai 2022 akitokea Asec Mimosas ya Ivory Coast ameuzwa Wydad kwa Sh2 bilioni. Aziz KI alitambulishwa na Wydad Mei 24, 2025 sambamba na nyota wengine wawili wapya waliojiunga kujiandaa na michuano ya Kombe la Dunia la Klabu inayoendelea nchini Marekani. Wachezaji wa kigeni waliopo Wydad ni mabeki wa kati Guilherme Ferreira (Brazil) na Bart Meijers (Uholanzi), kiungo mkabaji Mickal Malsa (Ufaransa), viungo washambuliaji Arthur Wenderroscky (Brazil), Pedrinho (Brazil), Stephane Aziz Ki (Burkina Faso) na Thembinkosi Lorch (Afrika Kusini). Wengine ni washambuliaji Omar Al-Somah (Syria), Samuel Obeng (Ghana), Seleman Mwalimu (Tanzania) na Cassius Mailula (Afrika Kusini) anayecheza kwa mkopo akitokea Toronto FC ambapo mkataba wake huo unatarajiwa kumalizika Agosti 1, 2025. WASIKIE YANGA Wakati sintofahamu ikiwa kubwa juu ya hatma ya Aziz KI ndani ya Wydad, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema kiungo huyo alipelekwa huko kwa mkopo. “Mkataba ambao Aziz KI aliusaini na Wydad wakati tunamuuza ni wenye vipengele viwili – miezi mitatu ya kwanza wanamuangalia, wakijiridhisha na kiwango watamuongeza kwa miaka miwili,” alisema Kamwe. Alisema kwa mujibu wa makubaliano, Julai 10, mwaka huu Wydad wanatakiwa kuwasiliana na Yanga juu ya ishu ya Aziz KI kuendelea kusalia huko. “Aziz Ki bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Yanga. Endapo watashindwana naye basi atarejea nchini na atakuwepo kwenye mchezo wetu wa kwanza wa kufungua msimu ujao kwenye Ngao ya Jamii.” The post KUHUSU ISHU YA AZIZ KI KUTAKIWA KUTEMWA WYDAD…..YANGA WAWAPA JIBU HILI WAARABU…. appeared first on Soka La Bongo.

HUYU HAPA MVP WA IVORY COST ALIYEZIGONGANISHA SIMBA, YANGA…..KESI KUFIKISHWA FIFA….

HUENDA hii isiwe taarifa nzuri kwa mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wakianza kuchekelea chinichini baada ya kuwahabarisha juu ya dili la straika wa ASEC Mimosas na MVP wa Ligi Kuu ya Ivory Coast (Ligue 1), Celestin Ecua lililobaki hatua chache kabla ya kutua Jangwani. Ndio, Yanga inadaiwa kuwa ipo hatua nzuri ya kumnasa Ecua aliyehusika na mabao 27 katika mechi 30 za ligi msimu ulioisha akifunga mabao 15 na kutoa asisti 12, lakini ghafla watani wao, Simba imedaiwa wameingiza mkono na kuibua utata mkubwa. Ipo hivi. Utata umeibuka katika mchakato wa mshambuliaji huyo baada ya kudaiwa, Simba imeamua kuingiza mkono katika dili la kujiunga na Yanga na wakati wowote sakata hilo linaweza kutua FIFA. Inadaiwa kuwa, Yanga na Simba zote zimefanya mawasiliano ya kutaka saini ya Ecua aliyekuwa akiitumikia Asec kwa mkopo kutoka Zoman FC na ilielezwa Yanga ilikuwa katika hatua nzuri ikiwamo kumtangulizia kabisa mkataba ili ausome kabla ya kuusaini. Taarifa zinasema kuwa, mabosi wa klabu ya Yanga na Simba kwa vipindi tofauti wamekuwa wakifanya mazungumzo na kampuni ya uwakala wa wachezaji na makocha ya WA Football. Hata hivyo, wakati mazungumzo hayo yakiendelea inaelezwa ghafla mabosi wa Yanga wakapita njia nyingine kuwahi saini ya Ecua na mambo yakaanza kutibuka na hasa baada ya menejementi hiyo kushtuka inataka kuzidiwa akili, lakini ikiendelea kuwasikilizia Simba wanaoendelea hadi sasa. Inadaiwa, Ecua alisaini mkataba Machi, 2025 na kusimamiwa na kampuni hiyo inayomilikiwa na raia wawili wa Morocco ambayo pia katika ukurasa wake wa Instagram ameandika anasimamiwa na Waarabu hao. Yanga ilikuwa kwenye hatua za mwisho kumpa mkataba mshambuliaji huyo baada ya kufikia makubaliano na Zoman, lakini kampuni inayommiliki imesema  kuwa endapo maku-baliano yatakamilika wataiburuza klabu hiyo na mchezaji FIFA kwa kumshawishi nyota huyo mwenye mkataba. Wakati Yanga iliwekewa mtego huo, Simba nayo inaendelea kusukuma dili hilo ikiwatumia Wamorocco hao ambao pia wanahusika na umiliki wa kiungo mshambuliaji wa Wekundu hao, Ellie Mpanzu. Simba inawatumia Waarabu hao kama fimbo ili kuwabadilisha akili Zoman na kuwageuza kisha kuinasa saini ya Ecua kirahisi kupitia mgogoro huo, ikizingatiwa kuwa katika pendekezo la kocha Fadlu Davids anahitaji straika wa maana ili kuimarisha eneo la ushambuliaji. Mmiliki wa kampuni hiyo ya WA Football, Anas El Amran aliyekiri kuwepo kwa mgogoro huo akisema wameshangazwa na hatua ya Yanga kutaka kuwazunguka kwenye mazungumzo ya usajili wa mshambuliaji huyo. “Ni kweli kuna hiyo shida, tulianza vizuri mazungumzo na kiongozi mmoja wa Yanga (anamtaja) lakini hapa kati akawa kimya, baada ya muda mchezaji akatufuata na kutueleza kumbe mazungumzo yanaendelea na Yanga wanamtumia meneja mwingine,” alisema Amran na kuongeza; “Tulimtafuta yule kiongozi (anamtaja), lakini bahati mbaya sana majibu yake hayakuwa mazuri kwetu, tukamwambia mchezaji awe makini maana tukishasikia ameshasaini Yanga tutafungua kesi dhidi yake na hiyo klabu. “Tuna mkataba na Ecua wa miaka miwili, ndio maana hata kwenye Instagram yake ameweka jina letu, kufanya mazungumzo yoyote nje na sisi sio sawasawa tutawashtaki Fifa na watatulipa fedha nyingi.” Alipoulizwa kuhusu kufanya na mazunguzo na Simba ili kumnasa nyota huyo, alisema; “Ni kweli tunaendelea na mazungumzo na klabu, nyingine mbili ni za hapo Tanzania na nyingine za Afrika Kaskazini, tutakazokubaliana nazo tutamshirikisha mchezaji na klabu yake tutamalizana dili.” The post HUYU HAPA MVP WA IVORY COST ALIYEZIGONGANISHA SIMBA, YANGA…..KESI KUFIKISHWA FIFA…. appeared first on Soka La Bongo.

KUELEKEA CHAN…..TAIFA STARS YAKIMBILIA MISRI ‘KUVUNJA NAZI’….

KIKOSI cha Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Julai 08 2025 kiliingia kambini Dar es Salaam kisha alfajiri ya kuamkia Julai 9 kimekwea pipa kuelekea nchini Misri kwa ajili ya kambi ya wiki tatu. Hivyo kuelekea CHAN mambo ni moto na maandalizi yanaendelea kwa kasi ikiwa ni mwendelezo wa ukarabati wa Uwanja wa Mkapa ambao upo tayari kwa asilimia kubwa kuelekea CHAN. Stars Agosti 02, 2025 itacheza mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Chan 2024 dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam. Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara ni Aishi Manula, Mohamed Hussen Zimbwe, Dickson Job. Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Serikali wamebainisha kuwa kwa kiasi kikubwa maandalizi yanakwenda vizuri kwa ajili ya mashindano hayo ya Chan. The post KUELEKEA CHAN…..TAIFA STARS YAKIMBILIA MISRI ‘KUVUNJA NAZI’…. appeared first on Soka La Bongo.

Muuguzi wa India asubiri kunyongwa Julai 16

China Yatoa Onyo Kwa Marekani Kuhusu Ushuru Mpya – Yaapa Kulipiza Kisasi

KUHUSU ISHU YA AZIZ KI KUTAKIWA KUTEMWA WYDAD…..YANGA WAWAPA JIBU HILI WAARABU….

HUYU HAPA MVP WA IVORY COST ALIYEZIGONGANISHA SIMBA, YANGA…..KESI KUFIKISHWA FIFA….

KUELEKEA CHAN…..TAIFA STARS YAKIMBILIA MISRI ‘KUVUNJA NAZI’….

Lastest News

Don't miss daily news

© Image Copyrights Title

Muuguzi wa India asubiri kunyongwa Julai 16

  • 10 Jul 2025
  • 36
© Image Copyrights Title

Kikwete, Ashiriki Mkutano Maalumu London

  • 10 Jul 2025
  • 57
© Image Copyrights Title

Miaka 39 Madarakani: Museveni Aidhinishwa Kugombea Tena

  • 09 Jul 2025
  • 48
Read more News

Burudani

Don't miss daily news

© Image Copyrights Title

ADONIJAH OWIRIWA ,  MTAYARISHAJI MKUU WA FESTAC ’77, ANASEMA

Lorem ipsum dosectetur adipisicing elit, sed do.Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur Nulla fringilla purus at leo dignissim congue. Mauris elementum accumsan leo vel tempor.

  • 18
Read all News
© Image Copyrights Title

ADONIJAH OWIRIWA ,  MTAYARISHAJI MKUU WA FESTAC ’77, ANASEMA

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 18
© Image Copyrights Title

BASATA YA WAJENGEA UELEWA WA MIFUMO KUSOMANA MAAFIA UTAMADUNI NA BIASHARA MARA 

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 13
© Image Copyrights Title

MAJALIWA: SANAA INAMCHANGO MKUBWA KATIKA KUKUZA UCHUMI

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 12
© Image Copyrights Title

CDQ HATIMAYE AMEZINDUA VISUALIZER YA WIMBO MAARUFU “SUWE”

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 12
© Image Copyrights Title

MTANZANIA MWANAMUZIKI KAMANDA RAS MAKUNJA KUTUNIKIWA TUZO YA “Ambassodor of African Culture” NCHINI UJERUMANI

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 12
© Image Copyrights Title

UZINDUZI WA HEINEKEN SILVER WATIKISA CHINI YA ARDHI KWA MBWEMBWE ZA KIPEKEE

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 9
© Image Copyrights Title

HEINEKEN SILVER YAVUNJA REKODI KWA UZINDUZI WA KIPEKEE MLIMANI CITY

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 10
© Image Copyrights Title

HEINEKEN SILVER ILIVYOANZA MAPINDUZI YA BURUDANI MJINI DAR

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 9
© Image Copyrights Title

TAMASHA LA SABASABA KUINUA UCHUMI WA UBUNIFU NA KUWEZESHA WASANII NA FAMILIA

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 11
© Image Copyrights Title

HEINEKEN SILVER YAPOKELEWA KWA SHANGWE 

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 11

Michezo

Don't miss daily news

© Image Copyrights Title

KUHUSU ISHU YA AZIZ KI KUTAKIWA KUTEMWA WYDAD…..YANGA WAWAPA JIBU HILI WAARABU….

Lorem ipsum dosectetur adipisicing elit, sed do.Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur Nulla fringilla purus at leo dignissim congue. Mauris elementum accumsan leo vel tempor.

  • 45
Read all News
© Image Copyrights Title

KUHUSU ISHU YA AZIZ KI KUTAKIWA KUTEMWA WYDAD…..YANGA WAWAPA JIBU HILI WAARABU….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 45
© Image Copyrights Title

HUYU HAPA MVP WA IVORY COST ALIYEZIGONGANISHA SIMBA, YANGA…..KESI KUFIKISHWA FIFA….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 49
© Image Copyrights Title

KUELEKEA CHAN…..TAIFA STARS YAKIMBILIA MISRI ‘KUVUNJA NAZI’….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 52
© Image Copyrights Title

KUHUSU MANULA KURUDI ZAKE AZAM FC…HII HAPA STORI NYUMA YA PAZIA ISIYOSEMWA….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 56
© Image Copyrights Title

ISHU YA MPANZU KUTAKIWA NA WAARABU …UKWELI WOTE HUU HAPA…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 62
© Image Copyrights Title

MNASEMA KIBU HAJAWIKA MSIMU HUU 🙄🙄..?HIZI HAPA TAKWIMU ZAKE ZA KUTISHA 😎😎…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 49
© Image Copyrights Title

TZS BILIONI 1.5 ZIPO MEZANI, JIUNGE NA LUCKY RUSH TOURNAMENT YA MERIDIANBET LEO

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 54
© Image Copyrights Title

BONASI YA KIBABE KUTOLEWA UKIBASHIRI NA GG&3+…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 38
© Image Copyrights Title

MAISHA YA CAMARA SIMBA HATARINI….MABOSI WAVUTANA ‘ABAKI AU ASEPE’….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 46
© Image Copyrights Title

MASHINE MPYA YA MABOA YANGA HII HAPA….DILI LAKE MPAKA SASA LIPO HATUA HII…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 55
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook