Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

BASATA YA WAJENGEA UELEWA WA MIFUMO KUSOMANA MAAFIA UTAMADUNI NA BIASHARA MARA 

  • 8
Scroll Down To Discover

Baraza la Sanaa la Taifa limeanza kuwajengea uelewa maafisa utamaduni na Mafisa Biashara wa mikoa na Halmashauri ili juu ya kusomana kwa mifumo ya AMISI kwa Basata na TAUSI kwa Serikali za mitaa ili kuondoa changamoto za Urasimishaji wa sanaa za wasanii na kuboresha utendaji katika Baraza hilo 

pamoja na mambo mengine Mafunzo hayo ya kusomana kwa mifumo niutekelezaji wa maelekezo ya Rais DKT Samia Suluhu Hassan aliyoyayotoa hivi karibuni 

Akizungumza katika Mafunzo ya Maafisa Utamaduni,Maafisa Biashara kaimu mkurugenzi Msaidizi wa Utafiti na Masoko Mrisho Mrisho alisema Mafunzo haya nikuwambusha kuwa Maafisa hao kuwa wanao uwezo wa kutambua kazi za Sanaa ambazo walikuwa hawazifahamu.

Wanao uwezo wakusaidia wasanii vikundi vya sanaa, wadau wa sanaa na wamilik wa miundombinu ya sanaa ikiwemo kumbi za starehe na Burudan kujirasimisha kupitia mfumo wa usajili na vibali( AMIS)

Pia kupitia Mafunzo haya Basata imeanza kukuza uulewa kwa Maafisa Utamaduni na Maafisa Biashara juu ya kusomana kwa mifumo ya AMIS wa basata na TAUSI kwa upande wa Serikali za mitaa.

“Tumekuja mara nakukutana na maafisa utamaduni na Maafisa Biashara lengo tunawajengea uwezo wa kuelewa mfumo na umhimu wa Urasimishaji katika Sekta ya sanaa”Alisema Mrisho Mrisho Kaimu mkurugenzi Msaidizi wa Utafiti na Masoko Basata.

Kwa upande wao baadhi ya Maafisa Utamaduni wamesema muunganiko huo utasaidia kuondoa urasimu baina ya wasanii na watumishi pamoja na vitendo vya rushwa.



Prev Post MAJALIWA: SANAA INAMCHANGO MKUBWA KATIKA KUKUZA UCHUMI
Next Post ADONIJAH OWIRIWA ,  MTAYARISHAJI MKUU WA FESTAC ’77, ANASEMA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook