Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Jab Yaendelea Kutoa Vitambukisho Kwa Waandishi Wa Habari Waliokidhi Vigezo

  • 37
Scroll Down To Discover

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari-JAB,  Wakili Patrick Kipangula akimkabidhi Kitambulisho cha Uandishi wa Habari (Press Card) Mkurugenzi Mtendaji wa Michuzi Media Group Muhidin Issa Michuzi kwa niaba ya Waandishi wengine wanaoendelea kupokea vitambulisho vyao baada ya kukidhi vigezo vya kisheria.
Akizungumza mara baada ya kumkabidhi kitambulisho hicho Wakili Kipangula amempongeza Michuzi na Waandishi wengine waliokwishakupokea vitambulisho vyao baada ya kukidhi vigezo huku akitoa wito kwa Waandishi ambao bado hawajapata vitambulisho vyao kuingia katika mfumo kuhakiki viambatisho walivyoweka kama vipo na vinafunguka kabla ya kupiga simu Bodi kuulizia hali ya maombi yao.
Amesema maombi mengi yana mapungufu ya viambatisho hivyo kutosoma, kuonekana kiambatisho kimoja, kujirudia kwa kiambatisho kimoja, kuweka vyeti visivyotambulika kisheria na wengine barua za utambulisho kutoambatishwa.



Prev Post Lukuvi: Wizara Zingine Ziige Mfano Wa Wizara Ya Afya Kuhamia Mtumba
Next Post Rais Ruto Asema Hatang’atuka Kwa Shinikizo la Maandamano
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook