Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mgombea Mwenza Nchimbi: CCM Imedhamiria Kuboresha Elimu, Maji Na Miundombinu Katavi

  • 3
Scroll Down To Discover

Mgombea mwenza wa kiti cha urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema kuwa endapo Watanzania watampa ridhaa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuongoza kwa muhula mwingine wa miaka mitano, serikali yake imedhamiria kuboresha elimu kwa kujenga sekondari mpya 11 pamoja na madarasa mapya 98 katika Halmashauri ya Mlele, mkoani Katavi.

Dkt. Nchimbi ametoa kauli hiyo leo, Septemba 10, 2025, ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni za urais kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Halmashauri ya Mlele, Dkt. Nchimbi akiendelea kunadi sera za CCM, amesema chama hicho pia kimedhamiria kutekeleza miradi 16 ya maji safi na salama katika eneo hilo.

“Sambamba na hayo, kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025–2030, tutaendelea kuboresha hali ya barabara pamoja na miundombinu mbalimbali kwa lengo la kuchochea zaidi maendeleo ya wananchi,” amesema Dkt. Nchimbi.



Prev Post SIMBA WALIVYOTAMATISHA TAMASHA LAO KIBABE JANA…VIFAA VIPYA MHHHHH……
Next Post Nic Na Benki Ya COOP Wasaini Mkataba Wa Ushirikiano Wa Kimkakati kwa Ajili Ya Kupanua Huduma Za Bima
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook