
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma, imeamuru mwanachama wa ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, aruhusiwe kuendelea na mchakato wa kurejesha fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika uamuzi uliotolewa leo, Septemba 11, 2025, Mahakama imebainisha kuwa zuio lililowekwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) dhidi ya Mpina, bila kumpa nafasi ya kusikilizwa, lilikiuka sheria na Katiba.
Shauri hilo lilikuwa Na. 21692/2025, ambapo walalamikaji walikuwa Bodi ya Wadhamini wa ACT-Wazalendo pamoja na Luhaga Mpina, dhidi ya INEC na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mahakama imeeleza kuwa uamuzi wa Tume uliotolewa Agosti 27, 2025, uliwaathiri moja kwa moja waleta maombi, hivyo wanapaswa kupewa fursa ya kurejesha fomu zao mara moja.
Hata hivyo, Mahakama imekataa ombi la walalamikaji la kulipwa fidia ya shilingi milioni 100, ikisema halina msingi wa kisheria.
Uamuzi huo umesomwa na Jaji Abdi Kagomba wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!