
Katika hali isiyotarajiwa, nyumba ya familia ya Mzee Kombo Mkabala iliyopo Mtaa wa Idrisa, Magomeni jijini Dar es Salaam, imevunjwa kufuatia mgogoro wa ardhi wa muda mrefu na kuifanya familia hiyo ikose makazi.
Tukio hilo limewaacha wakazi wake, akiwemo mjamzito Farashum Mfaume, wakiwa hawajui la kufanya.
Chanzo cha uvunjaji wa nyumba hiyo kimeelezwa kuwa ni mgogoro wa ardhi uliodumu tangu mwaka 1987, kati ya familia ya Mzee Kombo na mlalamikiwa ambaye anatajwa kuwa mmiliki halali wa eneo hilo.
Global TV imefika eneo la tukio na kufanya mahojiano na familia husika, wakiwemo baadhi ya waathirika akiwemo Farashum — mjukuu wa marehemu Mzee Kombo — pamoja na viongozi wa serikali ya mtaa huo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!