KISA AZIZ KI KUSEPA YANGA …HUKO SIMBA WATU NI TABASAMU MPAKA JINO LA MWISHO😅….

KITENDO cha Aziz KI kukubali dili la kutua Wydad, atakuwa anaweka kwenye waleti mshahara wa Sh72.3 milioni kwa mwezi. Ni mara mbili ya aliokuwa akilipwa Yanga. Kingine ni kwamba mkataba wa Aziz KI na Wydad utakuwa wa miaka miwili akianza kucheza michuano ya Klabu Bingwa Dunia itakayofanyika Juni 15, 2025 hadi Julai 13, 2025, huko Marekani. Sasa kuna habari mpya. Kocha wa zamani wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefichua kwamba klabu hiyo itakuwa imefurahia kwa kiasi kikubwa kuuzwa kwa staa huyo kwani enzi zake kulikuwa na jitihada za makusudi za kumsajili kwa namna yoyote ile ikashindikana. Na ameweka wazi kwamba ni mchezaji aliyekuwa akiwanyima raha zaidi Simba na hata kwenye vikao vikubwa enzi zake alikuwa akijadiliwa sana kutokana na madhara yake uwanjani. Robertinho aliyetimuliwa Simba baada ya kichapo cha mabao 5-1 cha mechi ya Dabi ya Kariakoo iliyopigwa Novemba 5, 2023, alisema kama kuna timu itakayokuwa imefurahi kuondoka kwa Aziz Ki ni Simba,kwani enzi akiinoa ilikuwa ikimpigia hesabu kumng’oa Yanga ili wapate utulivu. Robertinho ambaye ni raia wa Brazili, alisema; “Simba ilikuwa na mkakati mkubwa wa kumuondoa Aziz KI Yanga, kwa namna yoyote ile hata kumsajili, lakini ilikuwa inashindikana kutokana na msimamo na mkataba aliokuwa nao Yanga.” “Yanga imepoteza nguvu kubwa, lakini kwa kuwa wamefanya biashara hakuna shida na ninaamini mbadala wake utakuwa umepatikana ndio maana wamechukua maamuzi hayo,”aliongeza Kocha huyo aliyepigwa chini baada ya kipigo cha mabao 5-1 kwenye dabi. “Kwa bidii na uwezo wa Aziz KI hakuna timu atakayokwenda asipate namba ya kucheza, kwani kocha wa klabu yake mpya atakuwa amemsoma vyema, Waarabu wanapenda sana mchezaji mwenye akili ya kufunga na kutengeneza nafasi,”aliongeza. Robertinho ni mmoja ya makocha aliyelizwa na Aziz KI, kwani katika Dabi iliyomtibulia kibarua kiungo huyo alifunga mabao mawili na kuasisti bao moja, lakini alifunga pia katika ushindi wa 2-1 katika mechi ya marudiano ya msimu huo Simba ikiwa chini ya Abdelhak Benchikha na pia katika sare ya 1-1 kabla ya Robertinho kutoa Msimbazi akitokea Vipers ya Uganda. Pia alifunga bao wakati Simba ikishinda 3-1 na ilipolazwa 3-0 na Asec Mimosas katika mechi za Shirikisho Afrika 2022. Yanga imekubali kumuuza Aziz KI kwa kiasi cha Sh 2Bilioni, lakini mkataba ukiwa na kipengele cha kwamba kama atachemsha na kutaka kuondoka Wydad, basi Yanga itapewa kipaumbele. The post KISA AZIZ KI KUSEPA YANGA …HUKO SIMBA WATU NI TABASAMU MPAKA JINO LA MWISHO😅…. appeared first on Soka La Bongo.

ALICHOKISEMA FADLU BAADA YA SIMBA ‘KUNYONGWA CAF’ JUZI….

SIMBA imeumia. Mashabiki wamebeba majonzi. Viongozi wamesalia na maswali. Lakini katikati ya huzuni hii nzito, moto mpya unawashwa Msimbazi. Moto wa mageuzi. Moto wa kulipiza kisasi kwa njia ya mafanikio katika michuano ya CAF kwa msimu ujao wa 2025-2026. Hii imetokana na Simba kupoteza nafasi ya kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika mbele ya RS Berkane ya Morocco, licha ya kutoka sare nyumbani. Simba ilipoteza ugenini kwa mabao 2-0 hivyo kufanya matokeo ya mwisho kuwa kipigo cha mabao 3-1 na kuwanyima taji Wekundu hao kwa mara nyingine baada ya awali kulikosa Kombe la CAF katika fainali dhidi ya Stella Abdijan ya Ivory Coast. Kutokana na kukwama kuandika historia, benchi la ufundi, limewatuliza wanasimba kwa kuwaambia kuwa, wanaenda kujipanga upya na kurudi katika michuano hiyo msimu ujao wakiwa imara zaidi. Simba tayari imeshakata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao ikiwa na uhakika wa kumaliza nafasi mbili za juu za Ligi Kuu Bara msimu huu, baada ya kuikosa michuano hiyo na kuangukia Kombe la Shirikisho kutokana na kumaliza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu ya msimu uliopita. Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids hakuficha maumivu aliyonayo alipozungumza na moja ya gazeti la michezo nchini kwa sauti nzito yenye mchanganyiko wa uchungu na matumaini na kuwatia nguvu Wanasimba. “Tumepambana hadi mwisho. Tulikuwa na ndoto kubwa. Lakini mpira unafundisha. Sasa tunarudi nyuma kidogo… si kwa ajili ya kukata tamaa, bali kuchaji upya. Lazima tuwe tofauti msimu ujao,” alisema Fadlu anayekuwa kocha wa kwanza wa kigeni kuifikisha Simba fainali ya michuano ya CAF. Kocha huyo amesema wanaenda kujipanga na kutumia changamoto walizokutana nazo msimu huu kama njia ya kurudi kwa kasi na kufika mbali katika michuano hiyo ya kimataifa. Na kweli, tofauti hiyo inaanzia katika meza ya mipango. Tayari uongozi wa klabu kwa kushirikiana na benchi la ufundi umeandaa ramani ya usajili ramani inayoonesha bayana kuwa Simba haitaki tena kuwa mshiriki wa kawaida barani Afrika, bali bingwa halisi. Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu, Simba inatarajia kufanya usajili makini wa wachezaji watatu hadi wanne wa daraja la juu, wakilenga zaidi ubora kuliko idadi. Kiungo wa namba 10 ni kipaumbele. Ingawa Charles Jean Ahoua ameonesha kiwango kizuri, bado Simba wanahitaji mchezaji mwingine mbunifu, mwenye uwezo wa kusukuma mashambulizi, kutoa pasi za mwisho na kuamua matokeo kwa akili na ufundi. “Tunamheshimu Ahoua, lakini ili tuwe timu ya kutisha Afrika, hatuwezi kumtegemea mtu mmoja tu kwenye ubunifu. Tunahitaji mbadala wake, mshindani wake, au mshirika wake. Tunahitaji silaha zaidi,” alisema mmoja wa viongozi wa juu. Lakini kabla ya ndoto za Afrika, kuna kazi ambayo Simba inatakiwa kuifanya kwenye mashindano ya ndani kabla ya mapumziko kisha maandalizi ya msimu ujao. Simba sasa inajielekeza kikamilifu katika Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho (FA). Katika ligi, Yanga inaongoza kwa pointi 73, Simba ikifuata kwa pointi 69 huku ikiwa na mechi moja mkononi. Ushindi katika mechi hiyo ya kiporo unaweza tofauti ya pointi baina yao na Yanga huku kukiwa na mechi moja kati yao katika raundi tatu zilizopita. Katika Kombe la FA, Yanga tayari imeshafuzu fainali. Simba yenyewe inakibarua kutoka kwa Singida Black Stars mwishoni mwa mwezi huu. Ushindi kwenye nusu fainali hiyo utafungua ukurasa mwingine wa dabi ya fainali mechi ya heshima na ya kulipiza kisasi. Katika vikao vya ndani, viongozi wa Simba wameweka bayana dhamira yao: “Tunajenga kikosi cha fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, si cha Kombe la Shirikisho tena. Tumejifunza. Tumetambua mapungufu yetu. Na sasa tunarudi kwa kasi kubwa zaidi.” Mashabiki nao wameanza kurejeshewa matumaini. Kauli ya “Subirini muone Simba hatari zaidi si ya kutupwa hewani ni ahadi. Ni kiapo. Ni onyo kwa wapinzani ndani na nje ya nchi. Msimu huu haujaisha, lakini tayari Simba imeanza kuupamba msimu ujao kwa matumaini, mabadiliko, na ndoto ya kurudi katika ngazi ya fainali Afrika. Simba imefika fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kupoteza mechi mbili tatu katika hatua tofauti, lakini ikilinda rekodi ya kutopoteza mchezo wowote nyumbani, kwani imeshinda sita na kutoka sare moja tu iliyopata juzi kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar dhidi ya Berkane. The post ALICHOKISEMA FADLU BAADA YA SIMBA ‘KUNYONGWA CAF’ JUZI…. appeared first on Soka La Bongo.

MAGAZETI ya Leo Jumatano 28 May 2025

MAGAZETI ya Leo Jumatano 28 May 2025 MAGAZETI ya Leo Jumatano 28 May 2025 Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limewaita vijana waliomaliza kidato cha sita mwaka 2025 kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria kwa mwaka 2025. Kwa mujibu wa JKT, vijana hao wanatakiwa kufika katika makambi waliyopangiwa Kuanzia May 28 hadi June 8, 2025. Vijana hao wamepangiwa kuripoti katika makambi ya JKT Rwamkoma (Mara), Msange (Tabora), Ruvu na Kibiti (Pwani), Mpwapwa na Makutopora (Dodoma). Kambi nyingine za JKT ni Mafinga (Iringa), Mlale (Ruvuma)Mpambo na Maramba (Tanga), Makuyuni na Orjolo (Arusha), Bulombora, Kanembwa na Mtabila (Kigoma), Itaka (Songwe) Luwa na Milundikwa (Rukwa), pamoja na Nachingwea (Lindi). Aidha Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) waripoti katika kambi ya Ruvu iliyo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo. KUONA MAJINA BOFYA HAPA 

Ujio wa Teknolojia Mpya Kuchochea Ushiriki Kwenye Soko la Hisa

  MTENDAJI Mkuu wa Vertex International Securities limited Mateja Mgeta amewataka watu kuwekeza kupitia huduma ya Vertex Mobile Trading App ambayo itawasaidia wananchi kufanya uwekezaji kwa wepesi kwa kuwa ni moja ya njia nyepesi kwa watumiaji. Mateja amebainisha hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Vertex Mobile Trading App yenye lengo la kuwapa wepesi wawekezaji kupitia simu janja zao. Amesema lengo la ujio wa app hiyo una sura mbili ambazo ni kuwapa watu maarifa ya uwekezaji kwa urahisi iwe mtu anahitaji kuwekeza hisa katika makampuni yaliyoorodheshwa na soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) hivyo imani ni kubwa kuwa elimu ndio funguo ya ushiriki wa uwajibikaji. Sababu ya pili iliyowasukuma kuanzisha Vertex Mobile Trading App kulenga kurahisisha mfumo wa uwekezaji kuufanya uwe wazi, rahisi na salama kwa watumiaji ambao mwekezaji au mwekezaji mtarajiwa anayetumia simu janja (smart phone) anaweza kufungua akaunti ya hisa, kununua au kuuza hisa kupitia kiganjani pasipokuwa na ulazima wa kufika ofisni kwao. “Masoko ya mitaji yana jukumu muhimu sana katika kukusanya fedha kwa ajili ya matumizi yenye tija yanayotumika kama njia ambazo akiba inaweza kuelekezwa kwenywe miradi inayochochea ukuaji wa uchumi, ubunifu na kutengeneza ajira,”amesema Mateja. Aidha Mateja amesema uwekezaji uchangia kikamilifu katika ajenda ya uchumi wa Taifa, hivyo kutokana na uwekezaji unaweza kuimalisha masoko ya mitaji ya ndani, kupunguza utegemezi wa ufadhili kutoka nje na kukuza uwekezaji utakaochochea ustawi wa pamoja. Mateja ametoa pongezi kwa mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Tanzania (CMSA) chini ya Mtendaji wake Mkuu CPA Nicodemus Mkama kwa kuweka mazingira wezeshi katika soko kwani bila miongozo yao wasingeweza kufika walipo sasa. Pia alitoa pongezi kwa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) chini ya Afisa Mtendaji Mkuu Peter Nalitolela kwa mchango wao mkubwa kuhakikisha Vertex Mobile Trading App mafanikio ya hisa kiganjani ambayo yamefanywa na wao Vertex International Securities limited. Kwa upande wa mwakilishi kutoka CMSA Alfred Mkombo amesema wao mamlaka ya msoko ya mitaji wanafurahi kuona maendeleo kama haya ambayo yanawapa watu urahisi wa kuwekeza kupitia simu zao viganjani. “Simu imekuwa kitu kikubwa zipo hadi vijijini mtu anaweza kushiriki minada inayotokea Dar es Salaam bila kusafiri na kutumia gharama kubwa, Vertex Mobile App imetengenezwa ili kuleta mageuzi na ni tekinolojia ambayo inatumika kwa wepesi bila hata kutumia nguvu,” “Tunapenda kuona teknolojia hizi zinaleta tija zaidi tunawapongeza sana Vertex kwa namna ya kipekee kufikia hatua hii kubwa sana ya mafanikio ambayo inaakisi sera na sheria usimamizi unaoleta mazingira bora,”amesema Mkombo. Huku Ali Othman kutoka DSE amesema jambo lililofanywa na Vertex ni kubwa na litaleta mafanikio makubwa kwa kuwa ni njia nzuri na rahisi kwa watu kutumia. “App ina kila kitu kwa mtumiaji wa mtandao wowote Vertex Mobile Trading App imewarahisishia hii ni hatua nzuri inaongeza ushindani na ubunifu mpya kwa watu wote kuwekeza iwe mjini na hata vijini,”amesema Othman.  

Naibu Waziri Mkuu Biteko na Wadau Wajadili Fursa za Ushirikiano Sekta ya Madini

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Doto Biteko, akiwa kwenye picha ya pamoja na (kutoka kushoto) Bi. Fatma Abdallah (Mkurugenzi Mtendaji – Puma Energy Tanzania), Bw. Mark Russell (Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Puma Energy), Mh. Doto M. Biteko (Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati), Bw. Ben Ouattara (Mkuu wa Kanda ya Afrika – Puma Energy), na Dkt. James Andilile (Mkurugenzi Mkuu – EW) baada ya kikao cha kujadili fursa za ushirikiano katika sekta ya nishati. Tukio hilo lilifanyika leo katika ofisi za Waziri Mkuu, jijini Dodoma.

KISA AZIZ KI KUSEPA YANGA …HUKO SIMBA WATU NI TABASAMU MPAKA JINO LA MWISHO😅….

ALICHOKISEMA FADLU BAADA YA SIMBA ‘KUNYONGWA CAF’ JUZI….

MAGAZETI ya Leo Jumatano 28 May 2025

Ujio wa Teknolojia Mpya Kuchochea Ushiriki Kwenye Soko la Hisa

Naibu Waziri Mkuu Biteko na Wadau Wajadili Fursa za Ushirikiano Sekta ya Madini

Lastest News

Don't miss daily news

© Image Copyrights Title

Jela Miaka 30 Kwa Kumbaka Kiziwi Wilaya ya Kwimba, Mwanza

  • 09 Apr 2025
  • 32
© Image Copyrights Title

Diamond Athibitisha Kununua Gari Jipya ‘Bugatti’.

  • 08 Apr 2025
  • 25
© Image Copyrights Title

Viwanja Vya Thamani Zaidi Kuwahi Kujengwa Duniani.

  • 08 Apr 2025
  • 13
© Image Copyrights Title

Diva Adai Hawezi Kuishi Vijijini Kisa Anaomba Vumbi.

  • 08 Apr 2025
  • 11
© Image Copyrights Title

Travis Scott Kupiga Show Afrika Kusini Mwaka Huu 2025.

  • 08 Apr 2025
  • 11
© Image Copyrights Title

Jux Uso Kwa Uso Na D’Banj Mjini Lagos, Nigeria.

  • 08 Apr 2025
  • 11
Read more News

Burudani

Don't miss daily news

© Image Copyrights Title

Chris Brown ashitakiwa kwa kumshambulia mtu kwenye klabu ya Usiku

Lorem ipsum dosectetur adipisicing elit, sed do.Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur Nulla fringilla purus at leo dignissim congue. Mauris elementum accumsan leo vel tempor.

  • 41
Read all News
© Image Copyrights Title

Chris Brown ashitakiwa kwa kumshambulia mtu kwenye klabu ya Usiku

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 41
© Image Copyrights Title

D Voice Atarajia Kuachia Ep yake Mpya

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 47
© Image Copyrights Title

Bobby Shmurda Asitisha Tour Yake, Auza Tiketi 10 Tu Kila Mji.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 36
© Image Copyrights Title

Wasanii Wanaowania Tuzo Za BET 2025.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 26
© Image Copyrights Title

Diamond Mfalme Wa Youtube Africa.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 45
© Image Copyrights Title

Rihanna Na Asap Rocky Watarajia Kupata Mtoto Wa 3.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 42
© Image Copyrights Title

Yammi Aacha Na Label Ya Nandy ‘The African Princess’.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 49
© Image Copyrights Title

Mtuhumiwa Aliyemuibia Kim Kardashian Afariki Dunia Kabla Ya Kesi Kuanza.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 33
© Image Copyrights Title

Mtuhumiwa Aliyemuibia Kim Kardashian Afariki Dunia Kabla Ya Kesi Kuanza.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 22
© Image Copyrights Title

Jux Ashinda Tuzo Ya Msanii Bora Afrika Mashariki Kwenye The Headies Nigeria.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 37

Michezo

Don't miss daily news

© Image Copyrights Title

KISA AZIZ KI KUSEPA YANGA …HUKO SIMBA WATU NI TABASAMU MPAKA JINO LA MWISHO😅….

Lorem ipsum dosectetur adipisicing elit, sed do.Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur Nulla fringilla purus at leo dignissim congue. Mauris elementum accumsan leo vel tempor.

  • 39
Read all News
© Image Copyrights Title

KISA AZIZ KI KUSEPA YANGA …HUKO SIMBA WATU NI TABASAMU MPAKA JINO LA MWISHO😅….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 39
© Image Copyrights Title

ALICHOKISEMA FADLU BAADA YA SIMBA ‘KUNYONGWA CAF’ JUZI….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 26
© Image Copyrights Title

NANI KUKUPATIA MKWANJA WA MAANA LEO….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 32
© Image Copyrights Title

BAADA YA MAMBO YA CAF KUISHA….VITA IKO KWA AHOUA, DUBE NA MZIZE….DUA YA WOTE HII HAPA…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 35
© Image Copyrights Title

GATES OF OLYMPIA – MLANGO WA USHINDI UMESHAFUNGULIWA…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 46
© Image Copyrights Title

CHUKUA CHAKO MAPEMA LEO…ODDS ZA USHINDI HIZI HAPA…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 47
© Image Copyrights Title

MERIDIANBET YAPIGA HATUA KUBWA KATIKA ULINZI WA MAZINGIRA

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 43
© Image Copyrights Title

ODDS KUBWA ZA KUKUPATIA MSHIKO ZIPO MERIDIANBET…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 43
© Image Copyrights Title

WAKATI DR MWINYI AKIHAIDI MIL 260….HAYA HAPA MAMBO 5 YA KUIBEBA SIMBA KESHO…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 48
© Image Copyrights Title

AFRIKA KUSINI USO KWA USO NA TAIFA STAR….NGOMA KUCHEZWA UGENINI…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 30
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook