
Binti aitwaye Elizabeth Matei (26) anadaiwa kupotea tangu tarehe Julai 4, 2025 mara baada ya kuondoka nyumbani kwao eneo la Mbande Msewe, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Global TV, mama wa binti huyo, Eliza, amesema siku hiyo Elizabeth aliaga kuwa anakwenda kuombewa pamoja na rafiki yake, kutokana na kuwa alikuwa akisumbuliwa na mapepo kwa muda mrefu.
Tangu siku hiyo hajarejea nyumbani, na juhudi za familia kumtafuta bado zinaendelea.
Endapo utabahatika kumuona au kwa taarifa yoyote unaweza kuwasiliana na Familia kupitia namba 0693560909.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!