Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mwili Wa Mtoto Ramin Wakutwa Kisimani

  • 28
Scroll Down To Discover

Mtoto Ramin

Mtoto Ramin, mwenye umri wa miaka mitatu, ambaye aliripotiwa kupotea na taarifa zake kusambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, amekutwa akiwa tayari amefariki ndani ya kisima kilichopo nyumbani kwao mkoani Tabora.

Tukio hilo limekuja baada ya juhudi za muda mrefu kutoka kwa familia, majirani na watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao walikuwa wakisaidia kusambaza taarifa za kutoweka kwake.

Kwa mujibu wa baadhi ya ndugu wa familia pamoja na watu wa karibu, mwili wa mtoto huyo uligundulika ndani ya kisima jana Tarehe 20 July 2025.

Jeshi la Polisi mkoani Tabora, kupitia kwa Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) Richard Abwao, limetoa ufafanuzi kuhusu kifo cha Mtoto Ramin mwenye umri wa miaka mitatu, ambaye awali aliripotiwa kupotea na taarifa zake kusambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, mwili wa mtoto huyo umekutwa tayari umefariki ndani ya kisima kilichopo nyumbani kwao, mkoani Tabora.

Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.

https://www.youtube.com/live/B2f781_mOfo?si=n3wZ1BZgz6ge4XoI

 



Prev Post DCI Yaondoa Mashtaka ya Ugaidi Dhidi ya Boniface Mwangi
Next Post Nchi Za SADC Kuendelea Kuimarisha Mifumo Ya Kiusalama Kwa Usalama Imara Wa Kanda
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook