
Wananchi wa Kijiji cha Mgela, kilichopo wilayani Kilindi mkoani Tanga, wamekumbwa na taharuki baada ya mwili wa marehemu, ambaye ni mzee wa miaka 85 aliyefahamika kwa jina la Mohammed Mjaila na aliyekuwa amezikwa miezi miwili iliyopita kijijini hapo, kufukuliwa na kisha kukatwa kichwa na watu wasiojulikana.
Akizungumza kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi, amesema kuwa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, huku akibainisha kuwa hali ni shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!