Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Israeli yatishia kuwaua viongozi wa Hamas waliosalia Qatar

Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, ametishia kuwaua tena viongozi wa Hamas walioko nchini Qatar iwapo Doha haitawafukuza maafisa hao, na kusababisha majibu makali kutoka kwa serikali ya Qatar. Pamoja na ukosoaji huo wa kimataifa kuhusu shambulio lililotokea katika mji mkuu wa Qatar inaarifiwa kuwa Netanyahu hajatetereshwa kwa namna yoyote. Netanyahu amesema siku ya Jumatano kwamba mataifa yanapaswa “kuipongeza” Israel kwa mashambulizi yake ya mabomu na mauaji katika maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati. Kauli hizo zilitolewa siku moja baada ya Israel kufanya shambulio lisilo la kawaida ndani ya Qatar, kwa kuwalenga viongozi waandamizi wa Hamas walioko Doha, wakati mazungumzo kuhusu pendekezo la kusitisha mapigano lililoungwa mkono na Marekani yakiendelea. Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imelaani vikali kauli za Waziri Mkuu huyo wa Israeli, ikizitaja kama “jaribio la aibu … la kuhalalisha shambulio la kinyonge dhidi ya ardhi ya Qatar, pamoja na vitisho vya wazi vya kuvunja tena mamlaka ya kitaifa ya nchi.” “Netanyahu anafahamu vyema kuwa ofisi ya Hamas ilifunguliwa nchini Qatar katika muktadha wa juhudi za upatanishi zilizopigiwa chapuo na Marekani pamoja na Israel,” Taarifa hiyo imeeleza. “Kauli kama hizi si jambo la kushangaza kutoka kwa mtu anayejiegemeza katika misimamo mikali ili kupata ushindi wa kisiasa, huku akiwa anatafutwa na vyombo vya sheria za kimataifa, akikabiliwa na vikwazo vinavyozidi kuongezeka kila uchao hali inayozidi kumtenga katika jukwaa la kimataifa,” Taarifa hiyo iliongeza. Wakati hayo yakijiri, ikumbukwe kwamba ndani ya kipindi cha siku tatu pekee, Israel imefanya mashambulizi katika maeneo ya Gaza, Lebanon, Yemen, Syria, Tunisia na Qatar, huku ikiendeleza uvamizi wa kila siku katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na siku ya Jumatano, Israeli iliwaua watu 35 katika shambulio nchini Yemen.

SIMBA WALIVYOTAMATISHA TAMASHA LAO KIBABE JANA…VIFAA VIPYA MHHHHH……

TAMASHA la Simba Day limehitimishwa kwa mechi ya kirafiki wa kimataifa uliozikutanisha Simba dhidi ya Gor Mahia ya Kenya. Mchezo huo uliofanyika jana Septemba 10, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-0, huku ikilipa kisasi mbele ya Gor Mahia. Kisasi hicho Simba imelipa baada ya mara ya mwisho kukutana kwao Juni 10, 2018 katika fainali ya SportPesa Super Cup ambapo Gor Mahia ilishinda pia 2-0 kwa mabao ya Meddie Kagere dakika ya 6 na Jacques Tuyisenge dakika ya 55. Katika mchezo huo, Simba ilipata bao la kwanza dakika ya 6, baada ya Abdulrazack Hamza kuunganisha kwa kichwa mpira wa faulo uliopigwa na Jean Charles Ahoua. Bao hilo la mapema lilifanya mashabiki wa Simba waliojitokeza Uwanja wa Benjamin Mkapa kushangilia kwa nguvu na kuendelea kuwapa sapoti mastaa wao. Mbali na kushangilia bao hilo, pia ufundi wa baadhi ya mastaa wa Simba waliouonesha ndani ya uwanja wakiwemo wapya kama Naby Camara na Rushine De Reuck, ulikuwa kivutio tosha. Mwingine ni kipa Yakoub Suleiman aliyeingia dakika ya 31 kuchukua nafasi ya Moussa Camara. Wakati Simba ikiwa mbele kwa bao moja, Gor Mahia ilirudi mchezo na kupangilia mashambulizi, lakini eneo la ushambuliaji lililokuwa likiongozwa na Christopher Ochieng halikuwa makini. Kipindi cha kwanza, Simba ilikwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa bao 1-0. Iliporejea kipindi cha pili, Kocha Fadlu Davids alifanya mabadiliko ya wachezaji watatu, akiwatoa Chamou Karaboue, Jonathan Sowah na Kibu Denis, nafasi zao zikachukuliwa na Yusuph Kagoma, Elie Mpanzu na Steven Mukwala. Mukwala alitumia dakika tatu pekee akiwa uwanjani kufunga bao la pili lililoongeza furaha Msimbazi. Hata hivyo, mshambuliaji huyo ilipofika dakika ya 65, zikiwa ni dakika 20 tangu aingie, alitolewa na kuingia Seleman Mwalimu. Mbali na mabadiliko hayo, Fadlu pia aliwapa nafasi nyota wengine walioingia kipindi cha pili ambao ni Joshua Mutale, Morice Abraham, David Kameta ‘Duchu’, Vedastus Masinde, Wilson Nangu, Alassane Kante, Mzamiru Yassin, Alexander Erasto na Bashir Salum. Kwa ushindi huo, Simba imeendelea kuwa na wakati mzuri katika Tamasha la Simba Day tangu 2009 ambapo sasa imeshinda michezo 12 ya kirafiki. Katika historia ya michezo ya Simba Day kuanzia mwaka 2009 hadi sasa 2025, Simba imeshinda dhidi ya SC Villa (2009, 2013 na 2015), AFC Leopards (2016), Rayon Sports (2017), Asante Kotoko (2018), Power Dynamos (2019 na 2023), Vital’O (2020), St George (2022), APR (2024) na Gor Mahia (2025). Pia imetoa sare moja pekee dhidi ya Express mwaka 2010, huku ikipoteza michezo minne dhidi ya Victors (2011), Nairobi City Stars (2012), Zesco United (2014) na TP Mazembe (2021). The post SIMBA WALIVYOTAMATISHA TAMASHA LAO KIBABE JANA…VIFAA VIPYA MHHHHH…… appeared first on Soka La Bongo.

‎NGURAH: USHIRIKIANO WA COOP BANK NA NIC KUKABILIANA NA UKOSEFU WA BIMA KATIKA SEKTA YA KILIMO

Na Meleka Kulwa -Dodoma  ‎Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ushirika (Coop Bank), Godfrey Ng’urah, amesema ushirikiano kati ya benki hiyo na Shirika la Bima la Taifa (NIC) unalenga kujibu changamoto za muda mrefu za ukosefu wa bima mahsusi kwa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi nchini. ‎“Tutaangazia sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi pamoja na mnyororo wa thamani wa kilimo biashara. Tunaingia na bima zitakazojibu ukosefu wa bima katika sekta ya kilimo biashara. Kwa kushirikiana na NIC, tutatoa huduma hizi kwa niaba yao kwa wateja wetu,” amesema Ng’urah leo Jumatano, Septemba 10, 2025 jijini Dodoma wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kibiashara. ‎Aidha, Amesema kuwa zaidi ya asilimia 65–70 ya Watanzania wanaishi vijijini na uchumi wao unategemea kilimo, hasa kupitia vyama vya ushirika. Aidha, kuna zaidi ya vyama vya msingi vya kilimo 6,000 vyenye wanachama milioni 8 pamoja na vyama vya fedha (SACCOS) karibu 2,000 vyenye wanachama milioni 2. ‎Ng’urah amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Ushirika imechukua hatua ya kuwaunganisha wakulima zaidi ya milioni 10 walioko chini ya vyama vya ushirika ili waweze kunufaika na huduma za mikopo na bima ikiwemo Shirika la Bima la Taifa (NIC). Amebainisha kuwa lengo ni kuwawezesha wakulima kulinda uwekezaji wao na kuongeza tija katika kilimo kwa ujumla. ‎Pamoja na mchango mkubwa wa kilimo kwenye uchumi wa taifa, taarifa zinaonesha kuwa sekta hiyo imekuwa ikipata sehemu ndogo ya mikopo ya kifedha. Kati ya Shilingi trilioni 40 zilizotolewa kwa ajili ya mikopo nchini, ni trilioni 3.8 pekee ndizo zilizoelekezwa kwenye sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi na biashara zinazotokana na sekta hizo. ‎Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Abdi Mkeyenge, amesema kuwa shirika hilo limejipanga kusaidia ukuaji wa uchumi wa taifa kupitia uwekezaji wa ada za bima kwenye benki za biashara nchini. ‎“Benki hii ikiwa na nguvu basi vyama vyenyewe vitakuwa na nguvu na wamiliki watafaidika, lakini pia tunamwangalia mkulima wa chini ambaye anatakiwa kuinuliwa. Sekta ya kilimo ni muhimu sana kwa ukuaji wa uchumi wa nchi yeyote, hasa sisi ambao tumebarikiwa eneo kubwa la kufanya kilimo,” amesema Mkeyenge. ‎Amefafanua kuwa NIC inatoa huduma za bima za maisha, mali, ajali na majanga, pamoja na bima za credit life ambazo hulinda dhidi ya upotevu wa fedha, akisisitiza kuwa ushirikiano huo na Coop Bank ni mkakati wa “kubakisha uchumi ndani ya nchi” kupitia uwekezaji wa ndani. ‎Makubaliano hayo yanalenga kutoa huduma jumuishi za kifedha na bima kwa wakulima kupitia vyama vya ushirika, hatua inayotarajiwa kuongeza upatikanaji wa mitaji kwa shughuli za kilimo, kupunguza athari za majanga, na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa. ‎Ushirikiano huo unatarajiwa kuongeza wigo wa huduma za kifedha na bima hadi kufikia zaidi ya asilimia 65 ya Watanzania wanaojihusisha na kilimo vijijini, hatua inayotajwa kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya uchumi wa kilimo nchini.

Nimegandisha mayai yangu kwa sababu sijapata mpenzi

 Chanzo cha picha,HANDOUTMaelezo ya picha,Ellie Lambert amegandisha mayai yake kwa matumaini hapo baadaye atakutana na mtu au "kuwa katika hali ya kifedha ambapo ataweza kulea mtoto peke yake"Maelezo kuhusu taarifaAuthor,Amy Walker, Philippa Roxby & Rozina SiniNafasi,BBCSaa 6 zilizopitaIdadi ya watoto waliozaliwa Uingereza na Wales, kwa sasa iko chini zaidi tangu miaka ya 1970, takwimu rasmi zinaonyesha.Kiwango cha uzazi - hutazama ni watoto wangapi wanaozaliwa na kila mwanamke wakati wa miaka yake ya kuzaa – kwa sasa kiko chini zaidi katika rekodi.Uingereza sio nchi pekee yenye tatizo hilo - nchi nyingi zinakabiliwa na kupungua kwa uzazi na zingine zinafanya juhudi kubwa kuongeza uzazi.Nini kimesababisha kuanguka kwa uzazi? Kuna gharama kubwa ya kulea watoto, kufanya kazi na changamoto ya kupata mpenzi sahihi.Lakini pia kuna ushahidi kwamba vijana wengi hawana mpango wa kuwa na watoto kabisa – nje ya sababu hizo.BBC imezungumza na wanawake wawili na wanaume wawili wenye umri wa miaka thelathini - umri wa wastani ambapo kwa watu wa Uingereza na Wales wanakuwa wazazi - kupata mawazo yao juu ya suala hilo.Kari, 34: Bora kuasili mtotoChanzo cha picha,HANDOUTMaelezo ya picha,Kari na mpenzi wake Kaitlyn wameamua kutozaa kwa sababu ya gharamaKari Aaron Clark, mtafiti katika Chuo cha Uhandisi cha Royal, anapata pauni 53,000 kwa mwaka lakini anahisi hawezi kumudu kulea mtoto huko London.Miaka minne iliyopita, mshahara wake ulikuwa pauni 22,000 wakati akimaliza PhD yake.Mpenzi wake Kaitlyn, ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa PhD, ana matatizo sawa ya kifedha.Ina maana licha ya mshahara wa juu kwa wastani wa Kari, amepata wakati mgumu kuweka akiba kwa ajili ya nyumba - jambo ambalo anaamini ni muhimu kabla ya kuwa mzazi kwa sababu ya hali ya "kutokuwepo kwa uhakika" katika kukodi.Pia anataja gharama za malezi ya watoto. Kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya shirika la hisani la watoto Coram, wastani wa gharama ya kila wiki ya kupata mlezi wa muda wote kwa watoto chini ya miaka mitatu nchini Uingereza ni pauni 300, ikilinganishwa na karibu pauni 430 katikati mwa London.Kari anasema, Kaitlyn ana maoni kama yake na wote wana wasiwasi kuhusu athari za mabadiliko ya tabia nchi."Napendelea sana wazo la kuasili mtoto. Kwa njia hiyo ninamsaidia mtu ambaye tayari anahangaika," anasema."Ninaweza kuasili mtoto baada ya kupitia hatua ya malezi ya utotoni."Licha ya kukata tamaa kwa sasa juu ya uwezekano wa kuwa mzazi kibaolojia, Kari anasema "haondoshi uwezekano wa kuzaa moja kwa moja."Chris na Jemma 33: Kufunga kizaziChanzo cha picha,HANDOUTMaelezo ya picha,Chris Taylor ameamua kufunga uzaziDerevam Chris Taylor na mkufunzi wa mbwa Jemma Wrathmell kwa pamoja wanapata mapato ya pauni 60,000 na wamekuwa pamoja kwa miaka 11.Wanandoa hao, wanaoishi Wakefield huko West Yorkshire, wanasema: "Tulikuwa na mazungumzo ya kina kujadili mambo kama shule, gharama na malezi," anasema Gemma.Lakini hitimisho lilikuwa; gharama ni kubwa sana."Baada ya malipo ya bili zetu zote na mambo muhimu hakuna nafasi ya bajeti ya kumudu mtoto," anasema Chris.Kwa sababu hiyo, wamechukua uamuzi - Chris anatarajia kufunga uzazi, baada ya miaka mingi ya Gemma kuzuia mimba.“Baadhi ya watu wamesema utabadili mawazo, lakini wajue ni uamuzi wetu,” anasema Jemma.Ellie, 39: Nimegandisha mayaiEllie Lambert, anayeishi Sheffield, anataka kupata watoto lakini anasema hajapata mwenza anayefaa.Miaka miwili iliyopita, alitumia pauni 18,000 kwa mizunguko miwili ya kugandisha yai. "Nachanganyikwa, ni gharama kubwa kwa kitu ambacho kinaweza kisisababisha chochote," anasema.Anatarajia kuzitumia akikutana na mtu sahihi, au akifikia hali ya kifedha ambapo anaweza kuishi mwenyewe kwa usaidizi wa mtoaji mbegu.Ellie anasema ana wasiwasi kuhusu gharama ya kifedha kwa mzazi mmoja.Ripoti kutoka Child Poverty Action Group ya mwaka jana iligundua wastani wa gharama ya kulea mtoto hadi umri wa miaka 18 ni pauni 166,000 kwa wanandoa na pauni 220,000 kwa mzazi mmoja.Ingawa Ellie alidhani angekutana na mtu kufikia mwishoni wa umri wa miaka 20, "licha ya kuwa kwenye programu zote za kutafuta mpenzi, bado hajafanikiwa."Akiwa tayari ametumia akiba yake kugandisha mayai, anasema itamugharimu pauni 10,000 zaidi kutumia mbegu ili kupandikiza.Dami, 34: Hadi niwe tayariChanzo cha picha,HANDOUTMaelezo ya picha,Bi Olonisakin anasema hana "haraka" ya kupata watotoKwa Dami Olonisakin, mwendesha kipindi cha ngono na uhusiano anayeishi London, maboresho ya matibabu ya uzazi - kama vile kugandisha yai - "yanawapa wanawake "nafasi zaidi kuliko hapo awali."Kuwa mama, anasema, si jambo la "kulichukulia kirahisi.""Gharama za malezi ya watoto zinapanda, sera za uzazi zina kikomo, kimsingi wanawake wanapaswa kufikiria sana," anasema.Anasema hana haraka. "Sijisikii niko katika haraka ya kutulia na kupata watoto kwa sababu tu watu wanatarajia hilo," anasema.Badala yake anaangazia kazi yake baada ya kukulia katika kaya ambayo "haikuwa na chochote"."[Wazazi wangu] walijitahidi sana, lakini siku zote nimekuwa nikisema sitakuwa na mtoto hadi niwe tayari."Hali ya baadayeHaya yote yanaibua swali la kipi kitatokea siku zijazo - ikiwa watoto wachache ndio watazaliwa.Kupungua kwa viwango vya uzazi haliwahusu tu watu kuchelewa kuzaa, lakini pia mwenendo unaokua wa watu kutotaka kuzaa kabisa, anasema Brienna Perelli-Harris, profesa wa demografia katika Chuo Kikuu cha Southampton.Takwimu kutoka Utafiti wa hivi karibuni wa Uzazi na Jinsia nchini Uingereza, zinaonyesha watu wazima wasio na watoto hawana uhakika wa kupata watoto, huku robo ya wale wenye miaka 18 hadi 25 wakisema hawana uhakika au hawatakuwa na mtoto."Gen Z wana uwezekano mkubwa wa kutaka kuishi bila mtoto," anasema. "Hapo awali, lilikuwa jambo la ajabu - sasa linakubalika zaidi."Na hilo linatokana na mambo ya kiuchumi kama mapato, gharama za malezi ya watoto na ajira.""Baada ya muda mrefu, idadi ya watu itaanza kupungua," anasema Prof Perelli-Harris.Hivi ndivyo hali ilivyo nchini Uingereza na nchi zingine kama Uhispania na Italia, ambapo kiwango cha uzazi ni cha chini."Uhamiaji unaweza kuzuia kupungua kwa idadi ya watu au hata kubadili hali mambo," anasema Prof Perelli-Harris.

Israeli yatishia kuwaua viongozi wa Hamas waliosalia Qatar

SIMBA WALIVYOTAMATISHA TAMASHA LAO KIBABE JANA…VIFAA VIPYA MHHHHH……

‎NGURAH: USHIRIKIANO WA COOP BANK NA NIC KUKABILIANA NA UKOSEFU WA BIMA KATIKA SEKTA YA KILIMO

PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 11, 2025

Nimegandisha mayai yangu kwa sababu sijapata mpenzi

Lastest News

Don't miss daily news

© Image Copyrights Title

BASHIRI YAKO YA USHINDI WA TAJI LA EPL UNAMPA NANI?….

  • 22 Jul 2025
  • 135
© Image Copyrights Title

Ramaphosa Amfuta Waziri Kontrovershali wa Elimu ya Juu

  • 22 Jul 2025
  • 116
© Image Copyrights Title

Adaiwa Kumuua Mama Mkwe Kwa Kumkata Mapanga

  • 22 Jul 2025
  • 102
© Image Copyrights Title

Watumishi Wawili wa TRA Wafariki Katika Ajali Geita

  • 22 Jul 2025
  • 177
© Image Copyrights Title

Ajali Ya Ndege Ya Kijeshi Yauwa 19 Dhaka, Bangladesh

  • 22 Jul 2025
  • 153
© Image Copyrights Title

Rais Samia Aridhia Tanzania Kuandaa Miss World 2027

  • 22 Jul 2025
  • 140
Read more News

Burudani

Don't miss daily news

© Image Copyrights Title

USUSI WATAJWA KAMA FURSA YA AJIRA KWA VIJANA

Lorem ipsum dosectetur adipisicing elit, sed do.Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur Nulla fringilla purus at leo dignissim congue. Mauris elementum accumsan leo vel tempor.

  • 26
Read all News
© Image Copyrights Title

USUSI WATAJWA KAMA FURSA YA AJIRA KWA VIJANA

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 26
© Image Copyrights Title

GUMZO LA JIJI. KWA SASA NI AMARULA SUNDOWN SESSIONS

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 25
© Image Copyrights Title

MSANII BILL NASS ALIVYOWAIMBISHA WANANCHI KONDOA

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 36
© Image Copyrights Title

WAZIRI DKT. GWAJIMA AMWAKILISHA SPIKA WA BUNGE DKT. TULIA AKSON KWENYE HAFLA YA MISS UNIVERSE TANZANIA, 2025,

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 52
© Image Copyrights Title

WAZIRI MWITA AWATAKA WANAMITINDO KUIWAKILISHA VEMA NCHI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 96
© Image Copyrights Title

“KAMA WAO” YAINGIA MTAANI! MUGGA MO NA BANDO MC WAPIGA KAZI SAFI

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 186
© Image Copyrights Title

ADONIJAH OWIRIWA ,  MTAYARISHAJI MKUU WA FESTAC ’77, ANASEMA

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 72
© Image Copyrights Title

BASATA YA WAJENGEA UELEWA WA MIFUMO KUSOMANA MAAFIA UTAMADUNI NA BIASHARA MARA 

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 69
© Image Copyrights Title

MAJALIWA: SANAA INAMCHANGO MKUBWA KATIKA KUKUZA UCHUMI

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 66
© Image Copyrights Title

CDQ HATIMAYE AMEZINDUA VISUALIZER YA WIMBO MAARUFU “SUWE”

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 74

Michezo

Don't miss daily news

© Image Copyrights Title

SIMBA WALIVYOTAMATISHA TAMASHA LAO KIBABE JANA…VIFAA VIPYA MHHHHH……

Lorem ipsum dosectetur adipisicing elit, sed do.Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur Nulla fringilla purus at leo dignissim congue. Mauris elementum accumsan leo vel tempor.

  • 40
Read all News
© Image Copyrights Title

SIMBA WALIVYOTAMATISHA TAMASHA LAO KIBABE JANA…VIFAA VIPYA MHHHHH……

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 40
© Image Copyrights Title

KIKOSI KAMILI CHA SIMBA 2025/26….KAPOMBE, MPANZU WALIVYOIBUA SHANGWE KWA MKAPA….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 46
© Image Copyrights Title

RASMI….DUCHU ARITHI VYA ‘TSHABALALA’ SIMBA….KIKOSI KAMILI MSIMU 2025/26 HIKI HAPA…..

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 37
© Image Copyrights Title

BAADA YA KUIFUNGA GHANA JUZI…MSHAMBULIAJI MPYA AISHTUA YANGA….MABOSI WAKUNA KICHWA

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 35
© Image Copyrights Title

SIMBA DAY :-MBOSO ALIVYO ‘MBOSOA’ KWA MKAPA LEO….ALLY KIBA ASHINDWA KUJIZUIA KWA ‘UTAMU’….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 27
© Image Copyrights Title

SIMBA DAY 25: BAADA YA KUONA ‘VIBE’ LA MNYAMA LEO…MORRISON AIPA SIMBA KIFAA…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 33
© Image Copyrights Title

ALIYETOKA LIGI ‘DARAJA LA KWANZA’ ATOA AHADI YA MAKOMBE SIMBA….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 41
© Image Copyrights Title

KISA YANGA KUWA NA THAMANI YA BIL 100….UTATA WAIBUKA…HOJA NZITO IKO HAPA….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 37
© Image Copyrights Title

KWA MAGORI, BARBARA NA MKWABI…SAPRIZI MPYA SIMBA HII HAPA…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 36
© Image Copyrights Title

SIKU 6 KABLA YA KUKIPIGA NA YANGA…PIGO JINGINE SIMBA HILI HAPA……

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 6
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook