Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

SIMBA KWAZIDI KUJISAFISHA….BAADA YA ZIMBWE…MSAIDIZI WA FADLU ABWAGWA MANYANGA RASMI…

  • 40
Scroll Down To Discover

WAKATI Simba ikiendelea kutangaza orodha ya wachezaji watakaokuwa nje ya hesabu za timu hiyo kwa msimu ujao wakiwapa ‘Thank You’, kuna msaidizi mmoja wa kocha Fadlu Davids amejiondoa ghafla.

Aliyetangaza kujiondoa ni mtaalam wa takwimu za wachezaji, Culvin Mavunga aliyetangaza kuondoka ndani ya timu hiyo.

Mavunga aliyefanya kazi kwa miaka mitano Simba akitokea kwao Zimbabwe, ametangaza uamuzi huo kupitia ukurasa wake wa Instagram saa chache zilizopita.

Katika ujumbe huo, Mavunga amewashukuru mashabiki wa Simba, Bodi ya Wakurugenzi, na benchi la ufundi likiongozwa na Fadlu kwa namna alivyofanya nao kazi kwa ushirikiano.

“Ukurasa wangu na Simba umefika mwisho, imekuwa misimu mitano ya kuvutia, tulishindwa, tukashindwa na kutoa sare,” ameandika Mavunga.

“Pongezi zangu za dhati ziwaendee mashabiki wa Simba, nyie ni watu wa muhimu, Bodi na uongozi wa Simba, ahsante kwa kila jambo.

“Benchi la ufundi la Simba, upendo sana na ninyi ni familia daima, wachezaji wa Simba nawapenda sana familia, kocha Fadlu ahsante kwa mafunzo.”

The post SIMBA KWAZIDI KUJISAFISHA….BAADA YA ZIMBWE…MSAIDIZI WA FADLU ABWAGWA MANYANGA RASMI… appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post ILE ISHU YA GIBRIL SILLAH KUTUA YANGA ILIBAKI 🤏🏽🤏🏽 TU YANI….
Next Post HIZI HAPA ‘TRIKI’ ALIZOTUMIA ENG HERSI KUWAZUNGUKA SIMBA KUMPATA BALA CONTE…NI UMAFIA…
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook