Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Watumishi Wawili wa TRA Wafariki Katika Ajali Geita

  • 35
Scroll Down To Discover

Watumishi wawili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamefariki dunia Julai 20, 2025, saa 4 usiku, katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Bwawani Katoro, barabara ya Katoro–Chibingo, Wilaya ya Geita.

Ajali hiyo ilihusisha gari la Serikali aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba STM 3696, mali ya TRA Mwanza, lililoendeshwa na Julius Dismas (31), mkazi wa Mwananchi, Mwanza.

Waliofariki ni: Emmanuel Leonard (33) – Ofisa Forodha, Mwita John (28) – Ofisa Forodha, wote ni wakazi wa Buswelu, Ilemela – Mwanza.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, chanzo cha ajali ni uchovu wa dereva, aliyeshindwa kumudu gari, likapinduka na kusababisha vifo hivyo.

Polisi wanatoa pole kwa familia na kuwataka madereva kuchukua tahadhari, kupumzika kabla ya safari na kuzingatia usalama barabarani.



Prev Post Mtanzania Atelekezwa India, Aomba Msaada wa Matibabu – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook