
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata shehena kubwa ya dawa mpya ya kulevya aina ya Mitragyna Speciosa iliyokuwa ikiingizwa nchini kwa kujificha kama mbolea.
Shehena hiyo ilibebwa kwenye mifuko 756 yenye uzito wa jumla wa tani 18.5. DCEA imesema dawa hiyo, ambayo ni aina mpya sokoni, ilikuwa imepangwa kuingizwa na kusambazwa ndani ya nchi kwa njia haramu.
Uchunguzi zaidi unaendelea kubaini wahusika na mtandao unaohusika na biashara hiyo haramu.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!