
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua Dkt. Halima Jumaane Wagao kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Leseni za Biashara katika Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda. Dkt. Halima alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Maeneo Huru – ZIPA.
Taarifa ya leo Agosti 13, 2025 iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena A. Said imeeleza kuwa Rais Mwinyi amemteua Mussa Juma Abdalla kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Umwagiliaji katika Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo.
Kabla ya uteuzi Ndugu Mussa alikuwa ni Mhandisi Mwandamizi, Idara ya Umwagiliaji Zanzibar na uteuzi huo unaanza leo tarehe 13 Agosti, 2025.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!