Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Waziri Mkuu Akagua Mabasi, Miundombinu Ya Mradi Wa BRT Awamu Ya Pili

  • 15
Scroll Down To Discover

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Agosti 13, 2025 amekagua mabasi mapya kwa ajili ya awamu ya pili mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT-2) pamoja na miundombinu ikiwemo kituo kikuu cha mabasi hayo cha Mbagala Rangi tatu na kituo cha gerezani, jijini Dar es Salaam.

Katika ukaguzi huo, Mheshimiwa Majaliwa ametembelea ujenzi wa kituo maalum cha kujazia gesi kwa ajili ya mabasi hayo, kinachojengwa katika kituo cha Mbagala Rangi Tatu.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Waziri Mkuu amewaagiza waendeshaji wa mradi huo kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha maeneo yaliyobaki yatakayowezesha mradi huo kuanza kutoa huduma ndani ya mwezi huu.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu aliambana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) William Lukuvi, Naibu Waziri Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Zainab Katimba, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi pamoja na watendaji wengine wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na Chuo cha Taifa cha usafirishaji (NIT).

Mradi wa BRT-2 unatarajiwa kuongeza ufanisi wa usafiri wa umma jijini Dar es Salaam na kutoa huduma ya kisasa, salama na ya haraka kwa wananchi.

 



Prev Post Mtu mmoja amefariki, 4 wameokolewa katika ajali ya mgodi Tanzania, katika Dira ya Dunia TV
Next Post Rais Mwinyi Ateua Wakurugenzi Wapya Serikalini
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook