Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Mwinyi Ateua Wakurugenzi Wapya Serikalini

  • 12
Scroll Down To Discover

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua Dkt. Halima Jumaane Wagao kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Leseni za Biashara katika Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda. Dkt. Halima alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Maeneo Huru – ZIPA.

Taarifa ya leo Agosti 13, 2025 iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena A. Said imeeleza kuwa Rais Mwinyi amemteua Mussa Juma Abdalla kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Umwagiliaji katika Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo.

Kabla ya uteuzi Ndugu Mussa alikuwa ni Mhandisi Mwandamizi, Idara ya Umwagiliaji Zanzibar na uteuzi huo unaanza leo tarehe 13 Agosti, 2025.



Prev Post Waziri Mkuu Akagua Mabasi, Miundombinu Ya Mradi Wa BRT Awamu Ya Pili
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook