
Wakili wa utetezi, Dkt. Rugemeleza Nshala, amesema bado haijajulikana iwapo kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, itarushwa moja kwa moja (mubashara) au la.
Akizungumza baada ya kikao cha mahakama, Dkt. Nshala alifafanua kuwa uamuzi wa urushaji mubashara utabainika baada ya kikao kinachotarajiwa kufanyika Agosti 18, 2025, kufuatia kuahirishwa kwa shauri hilo.
Kesi hiyo, inayosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Franco Kiswaga, imezua mjadala mkali baada ya upande wa mashtaka kuomba matangazo ya mubashara yasitishwe. Sababu kuu iliyotolewa ni kulinda utambulisho wa mashahidi raia, hoja ambayo imepingwa vikali na upande wa utetezi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!