Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

MFUPA ULIOMSHINDA MACKY APEWA MAYANGA

  • 7
Scroll Down To Discover

UONGOZI wa Mbeya City umekata mzizi wa fitina kwa kumtangaza rasmi aliyekuwa kocha wa Mashujaa FC, Salum Mayanga, kuchukua nafasi ya Mecky Maxime, huku ukilenga kuibadili sura ya timu hiyo ndani ya muda mfupi uliosalia wa msimu.

Uamuzi huo unakuja siku chache baada ya Mbeya City kufanya mabadiliko makubwa ya benchi la ufundi, yakiwemo ya kumfuta kazi Mecky pamoja na wasaidizi wake, kufuatia kipigo kizito cha mabao 6-0 walichopata dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, matokeo yaliyozidisha presha kwa klabu hiyo.

Mayanga sasa anakabidhiwa jukumu zito la kuinusuru Mbeya City ambayo kwa sasa ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 17 baada ya kucheza michezo 19, hali inayoiweka kwenye hatari kubwa ya kushuka daraja endapo haitapata matokeo chanya katika mechi zijazo.

Changamoto hiyo inahitaji mbinu, nidhamu na mabadiliko ya haraka ndani ya kikosi, ambapo macho na matumaini ya mashabiki wengi sasa yanaelekezwa kwa Mayanga kuona kama ataweza kuibadili hali hiyo na kuirejesha timu kwenye ushindani.

Kocha huyo anatarajiwa kuanza kibarua chake kwa mtihani mgumu dhidi ya waajiri wake wa zamani, Mashujaa FC, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Aprili 30, 2026 kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwara, Manyara, mechi ambayo inaweza kuwa kipimo halisi cha mwanzo wa safari yake mpya.

The post MFUPA ULIOMSHINDA MACKY APEWA MAYANGA appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post BADO TANO, VITA YA KUSHUKA EPL ILIVYOANZA KUKOLEA
Next Post MPANGO MKUBWA YANGA WAANZA KUFICHUKA, USAJILI WENYE KISHINDO WAPANGWA MAPEMA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook