Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

‎MAKONDA: ACHENI KUBEZA NCHI, JENGENI TASWIRA CHANYA KUVUTIA FURSA

  • 6
Scroll Down To Discover

Na. John Bukuku- Dar es salaam 

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, imesaini mkataba wa kuwa mwenyeji wa mashindano ya 74 ya Miss World 2027, tukio Hilo lililofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es Salaam Aprili 20, 2026 limeshuhudiwa na Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo , Mhe. Paul Makonda, huku akisisitiza umuhimu wa Watanzania kulinda amani na kuitangaza vyema nchi yao.

‎Aidha,Amesema kuwa mashindano hayo yatakayodumu kwa siku ishirini na nane yataambatana na matukio mbalimbali, hivyo kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani.

‎Ameyabainisha hayo Aprili 20,2026 Jijini Dar es salaam, Aidha amebainisha kuwa kuchaguliwa kwa Tanzania ni matokeo ya uwepo wa amani, utulivu pamoja na vivutio vya utalii vinavyoifanya nchi kuvutia kimataifa licha ya ushindani kutoka mataifa mengine.

Pia ameongeza kuwa ni wajibu wa Watanzania kuacha tabia ya kubeza nchi yao hususan kwenye mitandao ya kijamii, badala yake wajenge taswira chanya itakayosaidia kuvutia wageni na fursa zaidi.

Amesema kuwa wageni wanaoiona Tanzania kama nchi bora na yenye fursa wanashangazwa na baadhi ya Watanzania wanaoizungumza vibaya nchi yao, hali inayoweza kudhoofisha juhudi za kuitangaza kimataifa.

Aidha amebainisha kuwa ujio wa matukio makubwa ya kimataifa kama Miss World na AFCON unaonesha imani kubwa ya dunia kwa Tanzania, hivyo kunahitajika mshikamano wa kitaifa katika kulinda sifa hiyo.

Pia ameongeza kuwa kila Mtanzania ana jukumu la kuitangaza nchi yake kwa vitendo na maneno ili kunufaika na fursa za kiuchumi zinazotokana na matukio hayo makubwa.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO APRILI 12, 2026
Next Post Serikali kuwarasimisha na kuwawezesha mama na baba lishe
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook