Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

BADO TANO, VITA YA KUSHUKA EPL ILIVYOANZA KUKOLEA

  • 7
Scroll Down To Discover

LONDON, ENGLAND: KUANZIA maumivu ya Jumamosi iliyopita hadi ahueni fulani wiki hii! Huu umekuwa ni msimu mgumu kwa mashabiki wa Tottenham Hotspur, lakini baada ya kuona timu ikiruhusu bao la kusawazisha katika dakika za jioni dhidi ya Brighton, angalau wanaweza kupumua kwa sasa kutokana na West Ham United kuvutwa shati juzi dhidi ya Crystal Palace.

Sare ya West Ham katika Uwanja wa Selhurst Park ina maana hali imebaki kama ilivyokuwa huku Spurs wakiwa bado pointi mbili kutoka kwenye mstari wa kushuka daraja wanapopambana kujinasua kwenye hatari hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1977. “Itaenda hadi mwisho kabisa, bila shaka. Sio tu chini tu ya msimamo wa Ligi bali pia juu,” anasema kocha wa West Ham, Nuno Espirito Santo.

“Msimu huu umekuwa wa ushindani mkubwa sana. Hatupati pointi kirahisi, tunacheza mechi. Tuna jukumu mbele yetu na lazima tuendelee.”Leeds United na Nottingham Forest walikuwa na wakati mzuri katika raundi iliyopita ya Ligi Kuu England wote wakipata ushindi muhimu nyumbani na kujiweka pointi nane na tano mbali na eneo la kushuka daraja, huku Wolverhampton Wanderers tayari wakiwa wameshuka na Burnley wakitarajiwa kufuata, kuna kibarua kizito timu nyingine.

ISHU YA MATOKEO

Kocha wa Spurs, Roberto De Zerbi, alikuwa na matumaini makubwa kuhusu nafasi ya timu yake kubaki ligi baada ya sare yao na Brighton Jumamosi, akisema timu yake “ina uwezo wa kushinda mechi tano mfululizo”.

Lakini licha ya imani hiyo, ushahidi wa msimu huu hauonyeshi timu inayoweza kufanya hivyo.

Spurs hawajashinda mechi yoyote kati ya 15 zilizopita za ligi, jambo linalomaanisha hawajapata ushindi wowote katika ligi kuu mwaka 2026 na wamepata ushindi mara mbili tangu Oktoba 26.

Wanalazimika kuifunga Wolves Jumamosi ili kuepuka rekodi mbaya zaidi ya klabu ya kutoshinda mechi nyingi mfululizo, iliyowekwa miaka 91 iliyopita kati ya 1934 na 1935.

Kwa upande mwingine, kiwango cha wapinzani wao katika vita ya kushuka daraja kinaonekana kuimarika.

Leeds wameshinda mechi mbili mfululizo na kujisogeza karibu na eneo salama, Nottingham Forest wana ushindi mara mbili katika mechi tatu zilizopita na hawajafungwa katika mechi tano, huku West Ham wakishinda mechi mbili kati ya tano zilizopita.

Tukiangalia kwa upana zaidi, West Ham wamekusanya pointi 19 katika mechi 12 zilizopita, Forest wana pointi 18 katika mechi 13 na Leeds pia wana pointi 18 lakini katika mechi 14. Tangu waifunge Crystal Palace Desemba 28, Spurs wamekusanya pointi sita katika mechi 15.

MECHI ZILIZOSALIA

Kila mwaka ratiba inapotangazwa hakuna shaka kwamba muda wa kukutana na timu fulani unaweza kuwa na athari kubwa katika kipindi chote cha msimu wa miezi 10.

Zikiwa zimesalia mechi tano, Spurs wataamini kwamba ratiba iliyobaki angalau kwenye makaratasi inawapa nafasi kubwa ya kubaki ligi kuu. Mechi inayofuata ni ugenini dhidi ya Wolves, ambao tayari wameshuka daraja.

Pia watakuwa na mechi ya nyumbani dhidi ya Leeds Mei 11, ambayo wataiona kama fursa nyingine nzuri, hasa kama Leeds watakuwa tayari wamejihakikishia usalama wao kwa kuifunga Burnley katika mechi yao iliyotangulia.

Hata mechi ngumu ugenini dhidi ya Aston Villa Mei 3 inakuja wakati mzuri kwa Spurs, kwani itachezwa katikati ya michezo miwili ya nusu fainali ya Europa League kwa timu hiyo.

Watakwenda kwa wapinzani wao Chelsea kabla ya kuikaribisha Everton katika siku ya mwisho ya msimu siyo mechi rahisi hizo, hasa kwa kuwa timu zote mbili zinaonekana kupigania nafasi ya michuano ya Ulaya. Lakini kutokana na ushindani ulivyo mkali, hilo ni jambo ambalo timu zote zinazopambana kuepuka kushuka daraja zitalazimika kukabiliana nalo. West Ham wataikaribisha Everton Jumamosi kabla ya kusafiri kwenda kucheza na Brentford na ratiba yao itakuwa ngumu zaidi watakapocheza na Arsenal Mei 10.

Hata kama Newcastle United imekuwa maji kupwa na maji kujaa, kucheza ugenini katika Uwanja wa St James Park siyo kazi rahisi na mechi yao ya mwisho nyumbani dhidi ya Leeds inaweza kuwa na umuhimu mkubwa.

Kwa upande wa Forest, wao wana ratiba ngumu zaidi, wakiwa na mechi za ugenini dhidi ya Chelsea na Manchester United mwezi Mei.

Mechi za nyumbani dhidi ya Newcastle na Bournemouth siku ya mwisho zinaweza kuwa muhimu sana, lakini kupata matokeo dhidi ya Sunderland Ijumaa kutasaidia kupunguza presha kabla ya kumaliza msimu.

The post BADO TANO, VITA YA KUSHUKA EPL ILIVYOANZA KUKOLEA appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post SIMBA KWENYE HATARI, PEDRO AANZA KUUNDA KIKOSI KIPYA
Next Post MFUPA ULIOMSHINDA MACKY APEWA MAYANGA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook