KOCHA Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves ameanza rasmi kukisuka kikosi chake kuelekea mchezo mkubwa wa Kariakoo Derby dhidi ya Simba, akilenga zaidi kuimarisha safu ya kiungo baada ya kukosekana kwa Mudathir Yahya.
Kukosekana kwa Mudathir, ambaye ni mmoja wa viungo muhimu ndani ya kikosi hicho, kumeibua maswali kwa mashabiki juu ya namna timu itakavyoweza kujipanga, lakini benchi la ufundi linaonekana kuwa na majibu tayari.
Pedro ameweka wazi kuwa licha ya pengo hilo, hana hofu kwani anaamini kikosi chake kina wachezaji wa kutosha wenye uwezo wa kuziba nafasi hiyo na kuendeleza ushindani bila kuyumba.
Amesema maandalizi yanaendelea vizuri, huku akitumia michezo ya Kombe la Muungano kama sehemu ya kujaribu mifumo tofauti na kuwapa nafasi viungo wake kuonyesha uwezo wao kabla ya mtanange huo mkubwa.
Kariakoo Derby inatarajiwa kuchezwa Mei 3, 2026, ambapo Yanga watakuwa ugenini kumenyana na wenyeji wao Simba, huku bado kukiwa na sintofahamu juu ya uwanja utakaotumika kwa mchezo huo.
Akizungumza kuhusu mipango yake, Pedro alisisitiza kuwa ana imani kubwa na kikosi chake, akibainisha kuwa wanaangalia ni nani ataweza kuchukua nafasi ya Mudathir na kuendeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Kocha huyo alihitimisha kwa kueleza kuwa mbali na lengo la kutetea ubingwa wa Kombe la Muungano, pia wanatumia mashindano hayo kama jukwaa muhimu la kuijenga timu imara itakayokuwa tayari kwa ushindani mkali dhidi ya Simba.
The post SIMBA KWENYE HATARI, PEDRO AANZA KUUNDA KIKOSI KIPYA appeared first on Soka La Bongo.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!