Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

IBENGE AKIRI PRESHA YA SIMBA, YANGA, AAHIDI MAPINDUZI

  • 8
Scroll Down To Discover

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge amesema hatakubali tena timu yake kuwa daraja la mafanikio kwa Simba na Yanga katika michuano ya Kombe la Muungano inayoendelea visiwani Zanzibar.

Azam FC wanatarajiwa kushuka dimbani leo kuwakabili KVZ katika mchezo wa hatua ya mtoano utakaopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, kuanzia saa 1:15 usiku.

Historia ya hivi karibuni haijawa nzuri kwa Azam FC katika mashindano hayo, ambapo mwaka 2024 walitinga fainali ya Kombe la Muungano lakini wakapoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Simba.

Mwaka 2025, walijikuta wakipoteza tena fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Yanga kwa mikwaju ya penalti, katika mchezo uliopigwa Pemba chini ya kocha huyo huyo, Ibenge.

Kutokana na kumbukumbu hiyo ya kupoteza fainali mbili visiwani humo dhidi ya wapinzani wao wakubwa, Ibenge amesema safari hii wamejipanga kuhakikisha wanabadilisha historia kwa kufanya vizuri na hatimaye kutwaa ubingwa.

Ameeleza kuwa anaheshimu ubora wa kila mpinzani, akianza na KVZ katika hatua ya mtoano, huku akisisitiza umuhimu wa umakini ili kuhakikisha wanapata ushindi na kutinga hatua ya nusu fainali.

Ibenge amesisitiza kuwa hawatarudia makosa ya nyuma, akibainisha kuwa kila mchezo kwao ni kama fainali na lazima waucheze kwa umakini mkubwa.

“Tumekuja Zanzibar mara mbili na tumeshindwa kuchukua kombe licha ya kufika fainali. Tunajua kila timu ni bora, lakini sisi pia ni timu bora na tunataka kushinda safari hii,” amesema Ibenge.

Ameongeza kuwa kila mchezaji aliyesafiri na kikosi hicho anaelewa malengo ya timu ni kutwaa ubingwa, akisisitiza kuwa Azam FC ni klabu kubwa ambayo haipaswi kubaki nyuma huku wapinzani wao wakipata mafanikio mbele yao.

The post IBENGE AKIRI PRESHA YA SIMBA, YANGA, AAHIDI MAPINDUZI appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post SIMBA YATINGA MUUNGANO KIVITA, BARKER ATOA SILAHA ZOTE
Next Post SIMBA KWENYE HATARI, PEDRO AANZA KUUNDA KIKOSI KIPYA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook