Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais wa Iran Atuma Barua ya Wazi Kwa Wamarekani Kuhusu Vita

  • 9
Scroll Down To Discover

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, ameandika barua ya wazi kwa umma wa Marekani akihoji iwapo vita vinavyoendelea kati ya nchi yake na Marekani vinaendana na kaulimbiu ya “America First”.

Katika ujumbe huo uliowekwa kwenye mtandao wa X, Pezeshkian aliuliza ni kwa namna gani maslahi ya wananchi wa Marekani yanahudumiwa na mzozo huo, akisisitiza kuwa sera ya “America First” inapaswa kuzingatia manufaa ya watu wa Marekani.

Pezeshkian pia alidai kuwa Iran katika historia yake ya kisasa haijawahi kuchagua njia ya uchokozi wala kuanzisha vita, akieleza kuwa mitazamo inayoifanya Iran ionekane kama tishio inatokana na maslahi ya kisiasa na kiuchumi ya mataifa makubwa. Alisisitiza kuwa hatua zinazochukuliwa na Tehran ni za kujilinda.

Katika barua hiyo, alitofautisha kati ya serikali ya Marekani na wananchi wake, akibainisha kuwa watu wa Iran hawana uadui na mataifa mengine, ikiwa ni pamoja na Marekani na nchi za Ulaya, akisema hilo ni sehemu ya maadili ya muda mrefu ya utamaduni wa Iran.

Kwa upande mwingine, Rais wa Marekani, Donald Trump, alielezea viongozi wa Iran kama “regime hatari zaidi” na kusisitiza kuwa Iran kupata silaha za nyuklia kutakuwa tishio lisilokubalika. Pia alidai kuwa uwezo wa kijeshi wa Iran umedhoofishwa kutokana na mzozo unaoendelea.

Barua hiyo ya Pezeshkian inakuja katika kipindi ambacho mvutano kati ya Iran na Marekani ukiendelea kushika kasi, huku viongozi wa pande zote mbili wakitoa kauli zinazokinzana kuhusu hali ya usalama na mustakabali wa eneo hilo.

  

The post Rais wa Iran Atuma Barua ya Wazi Kwa Wamarekani Kuhusu Vita appeared first on Global Publishers.



Prev Post Video: Mbunge John Nchimbi Ajilipua Sakata la Mafuta, Watumishi Wanaotumia Magari Binafsi
Next Post Video: Hoja Nzito za Eric Shigongo Bungeni, Kuhusu CAG, Uchumi
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook