Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Video: Watu 9 Wanusurika Kifo Baada ya Lori la Mafuta Kulipuka Morogoro

  • 48
Scroll Down To Discover

Watu tisa, wakiwemo askari watatu—wawili wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na mmoja wa Jeshi la Polisi—wamenusurika kifo kufuatia mlipuko wa lori la mafuta uliotokea katika eneo la Doma, kwenye barabara kuu ya Morogoro–Iringa.

Tukio hilo limetokea wakati wahusika walipokuwa wakifanya juhudi za kuhamisha mafuta kutoka kwenye lori hilo lililokuwa limepinduka.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, SSF Shabani Marugujo, amesema majeruhi wote wamekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu, huku baadhi yao wakihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na kuungua sehemu mbalimbali za miili yao.

The post Video: Watu 9 Wanusurika Kifo Baada ya Lori la Mafuta Kulipuka Morogoro appeared first on Global Publishers.



Prev Post Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt.James Andilile Atenguliwa – Video
Next Post Rais Samia Afanya Uteuzi, Utenguzi, Uhamisho wa Viongozi, Angellah Kizigha Ateuliwa Mbunge
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook