
Mbunge wa Jimbo la Buchosa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo, amechangia mjadala Bungeni mjini Dodoma leo Aprili 2, 2026, akizungumzia hali ya uchumi.
Katika mchango wake, Shigongo amesema hali ngumu ya uchumi duniani na nchini Tanzania inachangiwa na mzozo unaoendelea kati ya Iran na Israel, uliosababisha kupanda kwa bei ya mafuta na kuyumba kwa uchumi wa mataifa mbalimbali.
Kutokana na hali hiyo, ameiomba Serikali kujibana katika matumizi, hasa katika kipindi hiki kigumu, kwa kudhibiti upotevu wa mapato na kuwachukulia hatua kali wote watakaobainika kuhusika na ubadhirifu.
Aidha, amegusia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akisisitiza umuhimu wa kuchukua hatua stahiki dhidi ya wote watakaobainika kukiuka taratibu na kujinufaisha na mali za umma.
The post Video: Hoja Nzito za Eric Shigongo Bungeni, Kuhusu CAG, Uchumi appeared first on Global Publishers.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!