Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Sadi Mtangi Ahukumiwa Miaka 60 Jela Kwa Makosa Ya Kubaka Wanafunzi – Video

  • 4
Scroll Down To Discover

Mahakama ya Wilaya ya Mkinga, mkoani Tanga, Julai 17, 2025 imemhukumu Sadi Mtangi, mkazi wa Maramba, kifungo cha miaka 60 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili ya kubaka wanafunzi wawili wa kike wenye umri wa miaka 13 na 9.

Awali, ilielezwa mahakamani kuwa mtuhumiwa alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kuanzia tarehe 11 Agosti 2024 dhidi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Maramba na Shule ya Msingi Mapatano, wote wakazi wa Maramba.

Akisoma hukumu hiyo, Mheshimiwa Hakimu Deda alisema kuwa mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kumhukumu mtuhumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kila kosa, adhabu itakayotekelezwa mfululizo.



Prev Post TLS Yapinga Ufafanuzi wa Zuio la Mahakama Dhidi ya Viongozi wa CHADEMA
Next Post Burkina Faso Yaivunja Tume ya Uchaguzi, Yahamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook