Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Burkina Faso Yaivunja Tume ya Uchaguzi, Yahamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani

  • 4
Scroll Down To Discover

Serikali ya kijeshi ya Burkina Faso imechukua hatua ya kuivunja rasmi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CENI), ikiituhumu kwa kuwa chanzo cha matumizi mabaya ya fedha za umma. Hatua hiyo imetangazwa kupitia runinga ya serikali ya RTB, ambapo ilielezwa kuwa jukumu la kusimamia chaguzi litawekwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

Uamuzi huu unakuja katika muktadha wa mabadiliko makubwa yanayoendeshwa na utawala wa kijeshi ulioko madarakani tangu Septemba 2022, ukiongozwa na Kapteni Ibrahim Traoré. Tangu walipochukua uongozi kupitia mapinduzi ya kijeshi, viongozi hao wameahirisha uchaguzi uliotarajiwa kufanyika mwaka uliopita, na kuongeza muda wa mpito hadi Julai 2029. Hii inamwezesha Kapteni Traoré kuendelea kuongoza na pia kuwania urais katika uchaguzi ujao.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la habari la AFP, Waziri wa Utawala wa Wilaya, Emile Zerbo, alisema kuwa tume hiyo ilikuwa ikigharimu serikali kiasi cha dola za Kimarekani 870,000 kwa mwaka. Alisisitiza kuwa kuiondoa tume hiyo kutasaidia “kuimarisha udhibiti wa serikali juu ya mchakato wa uchaguzi na kupunguza ushawishi wa kigeni.”

Hatua hii inazua wasiwasi miongoni mwa wachambuzi wa siasa na watetezi wa demokrasia, ambao wanaiona kama njia ya kuzuia kurejea kwa utawala wa kiraia na kudhibiti ushindani wa kisiasa nchini humo.



Prev Post Sadi Mtangi Ahukumiwa Miaka 60 Jela Kwa Makosa Ya Kubaka Wanafunzi – Video
Next Post Mfahamu Wakili Bagachwa Na Maono Ya Kuiona Missenyi Mpya
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook