Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mahakama Yamsimamisha Kazi Waziri Mkuu Thailand

  • 57
Scroll Down To Discover

Waziri Mkuu wa Thailand, Paetongtarn Shinawatra.

Mahakama ya Katiba ya Thailand imemsimamisha kazi Waziri Mkuu, Paetongtarn Shinawatra, kufuatia sakata la kisiasa lililosababishwa na uvujishaji wa mazungumzo yake ya simu na kiongozi wa zamani wa Cambodia, Hun Sen.

Katika klipu hiyo iliyosambaa kwa kasi, Paetongtarn alionekana akimwita Hun Sen “mjomba” na kutoa kauli za kumkosoa kamanda wa jeshi la Thailand jambo lililoibua hasira kubwa kwa wananchi na kupelekea wito wa kumwondoa madarakani. Wananchi wengi waliwasilisha maombi rasmi ya kutaka afutwe kazi.

Mahakama hiyo sasa inashughulikia rasmi kesi ya kumvua madaraka, huku Paetongtarn akipewa siku 15 kuwasilisha utetezi wake. Uamuzi wa Mahakama wa kumsimamisha kazi umefikiwa kwa kura 7-2. Kwa sasa, Naibu Waziri Mkuu Suriya Jungrungruangkit ndiye anayeshikilia nafasi ya kaimu waziri mkuu.

Paetongtarn ni mwanasiasa wa tatu kutoka katika familia ya Shinawatra ambayo imetawala siasa za Thailand kwa zaidi ya miaka 20 kupoteza madaraka kabla ya kumaliza muda wake.

Tukio hili linatokea wakati muungano wa Pheu Thai ukikumbwa na misukosuko, baada ya mshirika wake mkuu wa kihafidhina kujiondoa wiki mbili zilizopita, hali iliyopunguza idadi ya wabunge wa muungano huo bungeni.

Iwapo Mahakama itaamua kumvua rasmi madaraka, Paetongtarn atakuwa waziri mkuu wa pili kutoka chama cha Pheu Thai kuondolewa ofisini tangu Agosti mwaka jana—ishara ya mvutano unaoendelea kati ya vyombo vya dola na familia ya Shinawatra.



Prev Post Kesi Ya Tundu Lissu Yaahirishwa Hadi Julai 15, 2025 – Video
Next Post Wakili Oscar Mutaitina Ajitosa Kuwania Ubunge Jimbo la Bagamoyo
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook