
Wakili maarufu, Oscar Oswald Mutaitina, amejiunga rasmi katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Bagamoyo, baada ya kuchukua fomu ya uteuzi kuwania nafasi hiyo. Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Mutaitina amesema kuwa uamuzi wake umetokana na nia ya dhati ya kutaka kuyatumikia kikamilifu wananchi wa Bagamoyo na kutatua changamoto ambazo kwa muda mrefu zimekuwa kikwazo kwa maendeleo yao.
Ameeleza kuwa anaamini katika uongozi wa uwazi, ushirikishwaji na uwajibikaji, na kwamba endapo atapata ridhaa ya wananchi, atahakikisha anasimamia kikamilifu utekelezaji wa sera na mikakati ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, miundombinu na ustawi wa jamii.
“Nimeamua kugombea ubunge kwa sababu naamini bado kuna mambo mengi yanayohitaji kushughulikiwa kwa uharaka katika Jimbo letu. Ninataka kuwa sauti ya wananchi bungeni na daraja la kweli kati ya Serikali na watu wake,” alisema Mutaitina kwa msisitizo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!