Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kesi Ya Tundu Lissu Yaahirishwa Hadi Julai 15, 2025 – Video

  • 68
Scroll Down To Discover


Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, imeendelea kusuasua baada ya kuahirishwa tena hadi Julai 15, 2025, kutokana na hatua ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kutokamilisha mapitio ya jalada la kesi hiyo. Kwa mujibu wa Mawakili wa Jamhuri, faili la kesi bado lipo mezani kwa DPP na uchunguzi haujakamilika.

Katika kikao kilichofanyika leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Lissu, kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, aliomba mahakama iielekeze Jamhuri kutoa taarifa ya kina kuhusu hatua ya uchunguzi, akieleza kuwa ni haki yake kujua kinachoendelea. Alisisitiza kuwa hadi kufikia wiki ijayo, atakuwa amekaa mahabusu kwa siku 90, bila kesi kusikilizwa wala mashitaka rasmi kuanza kusikilizwa kwa kina.



Prev Post Rais Samia Amteua Gilead Teri Kuongoza Mamlaka Mpya ya Uwekezaji (TISEZA)
Next Post Mahakama Yamsimamisha Kazi Waziri Mkuu Thailand
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook