Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Sekretarieti Ya Halmashauri Kuu CCM Yakutana Kufuatilia Mchakato Wa Fomu Za Uteuzi

  • 9
Scroll Down To Discover

Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, imekutana katika kikao chake maalum leo Jumamosi tarehe 28 Juni 2025, kufuatilia mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi ndani ya CCM.

Kikao hicho kilipokea na kufuatilia kwa karibu taarifa mbalimbali za zoezi hilo la uchukuaji wa fomu za kuwania uteuzi wa kugombea nafasi za uwakilishi katika vyombo vya dola, lililoanza rasmi leo kwa mchakato wa ndani ya CCM, katika maeneo yote nchi nzima.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa awali, ratiba ya kuchukua na kurejesha fomu hizo za kuwania kuteuliwa ndani ya CCM, imeanza *leo tarehe 28 Juni 2025, saa 2:00 asubuhi na itahitimishwa tarehe 2 Julai 2025, saa 10:00 jioni.*

Ratiba hiyo itahusisha uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi nafasi za; Ubunge wa Jimbo, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, Ubunge wa Viti Maalum, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Viti Maalum, Udiwani wa Kata au Wadi na Udiwani wa Viti Maalum.



Prev Post Makonda Achukua Fomu Ya Ubunge Jimbo La Arusha Mjini Kupitia CCM
Next Post Ajali Mbaya Yahusisha Mabasi Mawili Yaliyogongana Uso Kwa Uso Same
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook