
Same, Kilimanjaro – Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea leo katika eneo la Sabasaba, kata ya Same, wilayani Same, mkoani Kilimanjaro, ambapo basi la abiria la kampuni ya Channel One lililogongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Coaster.
Basi la Channel One lilikuwa likisafiri kutoka Moshi kuelekea Tanga, huku basi dogo la Coaster likitokea wilayani Same. Baada ya kugongana, magari yote mawili yalishika moto na kuteketea kwa kiasi kikubwa, hali iliyozua taharuki kubwa kwa mashuhuda wa tukio hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa:
“Tunaendelea na juhudi za uokoaji kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama. Lengo ni kunusuru waliobaki hai na kutoa miili ya wale waliopoteza maisha katika ajali hii ya kusikitisha.”
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!