Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Chuo Kikuu Cha Kampala (KIUT) Chang’ara Fainali Ya Ubingwa Mpira Wa Wavu (DAREVA)

  • 39
Scroll Down To Discover

Wachezaji wa timu ya wanaume pamoja na mchezaji wa timu ya wanawake ya mpira wa wavu kutoka Chuo Kikuu cha Kampala (KIUT), wakionyesha vikombe vyao kwa fahari baada ya ushindi mkubwa kwenye mashindano

Timu za Mpira wa Wavu (Volleball) wanawake na wanaume, za Chuo Kikuu cha Kampala kilichopo Jijini Dar es Salaam, zimetangazwa mabingwa wa Mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es Salaam, (DAREVA), katika fainali ya mashindano, yaliyohitimishwa jana katika Uwanja wa michezo wa Chuo Kikuu hicho.

Katika kuwasaka mabingwa hao, timu ya KIUT wanawake, ilifanikiwa kuichapa timu ya Bandari ya Dar es Salaam, (TPA), kwa seti 3-1, wakati timu ya wanaume wa Chuo hicho, KIUT, walifanikiwa kutwaa ubingwa kwa kuichapa timu ya High Voltage seti 3-0.

Katika mashindano hayo, mshindi wa kwanza kwa timu zote za wanawake na wanaume walipata kikombe, medali na fedha taslimu Sh.1,000,000 kwa kila timu, ambazo zote zilibaki katika timu za KIUT.

Timu ya wanawake, Mpira wa Wavu (Volleball), ya Chuo Kikuu Cha Kampala (KIUT)

Aidha, katika matokeo hayo timu ya TPA wanawake ilifanikiwa kushika nafasi ya pili na kuchukuwa medali na Sh. 500,000 huku timu ya Voltage wanaume ikishika nafasi ya pili kwa zawadi hizo.

Akiongea baada ya kumazika kwa michuano hiyo, mgeni rasmi wa fainali hiyo, Rais wa Shirikisho la Mpra wa Wavu Tanzania (TVF), Mhandisi Magoti Mtani amesema kuwa, mafanikio ya mashindano hayo yametokana na jitihada zilizofanywa na viongozi waliopambana katika kuandaa ligi hiyo.

“Mafanikio haya nimatokeo mazuri ya jitihada za viongozi pamoja na Mameneja ambao walihakiakisha timu zinafika uwanjani, pamoja na hali ngumu ambayo wakati wingine walilazimika kutumia fedha zao, hii yote ni kutokana na mapenzi wa michezo huo,” amesema Mhandisi Magoti.

Amewashukuru wadhamini wachache waliojitokeza lakini pia amewaomba wadhamini kujitokeza kwa wingi na kujiunga na DAREVA ili kudhamini mchezo huo.

Mashabiki wakifuatilia kwa hamasa kubwa michezo ya mpira wa wavu ikiendelea

“Pia napenda wachezaji mtambue kuwa ligi yetu itaendelea tena na itaanza rasmi 25,Julai, 2025 katika viwanja vile vile vya nyumbani, Mwembe Yanga, na tunatarajia mechi zote zitakwenda mubashara kwenye kituo cha televisheni cha Azam na zitakazokosa nafasi, zitarushwa kwenye chaneli za Utube,” ameongeza.

Kufuatia maandalizi ya mashindani hayo, amewataka viongozi wa timu kuhakikisha wanasajili timu zao ili kuweka umakini zaidi na kujiwekea thamani na uhakikika kwa wadhamini hao wanaojitokeza.

Wachezaji wa timu ya wanaume pamoja na mchezaji wa timu ya wanawake ya mpira wa wavu kutoka Chuo Kikuu cha Kampala (KIUT), wakionyesha vikombe vyao kwa fahari baada ya ushindi mkubwa kwenye mashindano

Mwisho.

🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.



Prev Post Serikali Kusaidia Matibabu Kwa Kaya Zisizokuwa Na Uwezo Kupitia Bima Ya Afya Ya NHIF
Next Post Fadlu: Tuna Mechi Moja Tukishinda Tutakuwa Mabingwa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook