Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Fadlu: Tuna Mechi Moja Tukishinda Tutakuwa Mabingwa

  • 47
Scroll Down To Discover

Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids

Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids ameweka wazi kuwa wana mchezo mmoja mkononi ambao wakishinda watakuwa mabingwa.

Mchezo huo ni dhidi ya Yanga SC ambao unatarajiwa kuchezwa Juni 25 2025, Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mzunguko wa pili msimu wa 2024/25.

Simba SC katika mchezo wa raundi ya 30 ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar likifungwa na Steven Mukwala inafikisha pointi 78 nafasi ya pili na vinara ni Yanga SC wenye pointi 79.

Mchezaji wa Simba SC Awesu Awesu kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar

Fadlu amesema walipata kazi kubwa mbele ya Kagera Sugar hivyo mchezo mmoja uliobaki wakishinda watakuwa mabingwa wa ligi kuu ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.

“Tumepata pointi tatu mbele ya Kagera Sugar unaona haukuwa mchezo mwepesi kwetu, tuna mchezo mmoja ambao tukishinda tutakuwa mabingwa.”

Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.



Prev Post Chuo Kikuu Cha Kampala (KIUT) Chang’ara Fainali Ya Ubingwa Mpira Wa Wavu (DAREVA)
Next Post Meridianbet Foundation Yaadhimisha Miaka Mitano ya Msaada wa Masomo Duniani
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook