Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Michuano ya CDF CUP Kuanza Kutimua Vumbi Julai 2

  • 10
Scroll Down To Discover

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Stergomena Lawrence Tax (Mb) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mashindano ya kombe la Mkuu wa Majeshi Tanzania (CDF CUP) 2025.
Lengo kuu la mashindano hayo limetajwa kuwa ni kujenga ushirikiano, upendo, undugu na uzalendo miongoni mwa wanajeshi na raia.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi Julai, 2, mwaka huu 2025 ambapo yataendelea mpaka 14, Julai, 2025, Jijini Dar-es-Salaam. Imeelezwa kuwa mwaka huu mashindano hayo yatakuwa na ushindani mkubwa tofauti na miaka ya nyuma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo, Brigedia Jenerali Saidi Hamisi Saidi.
Akizungumza na wanahabari mapema leo, jijini Dar-es-Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano hayo, Brigedia Jenerali Saidi Hamisi Saidi, amesema Maandalizi yote ya kombe hilo yameshakamilika.
Ameendelea kusema kuwa mashindano hayo kwa muhula wa kwanza yalianzishwa mwaka 2014 na yalifanyika kwa mihula mitano hadi mwaka 2018.
Mkutano ukiendelea.
Aidha, kwa kutambua umuhimu wa michezo hiyo na kwa uzito wa pekee michezo ilirejeshwa na kuanza kufanyika tena kuanzia mwaka jana (2024) ambapo sasa yatakuwa yanafanyika kila mwaka.
“Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob John Mkunda  (CDF CUP) kwa mwaka huu yanatarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe Julai 2,  25 hadi tarehe 14 Julai, 25, na  Kauli mbiu ya michezo hii ni CDF CUP 2025 – MICHEZO NI UMOJA NA MSHIKAMANO.
“Mashindano ya Michezo ya Kombe la Mkuu wa Majeshi yameanzishwa kwa madhumuni ya kuwakutanisha wanajeshi wote nchini kutoka kila Kamandi ya Jeshi ya Ulinzi la Wananchi Tanzania ambao ni Maafisa, Askari pamoja na Watumishi wa umma.
Burudani ya ngoma ikiendelea.
“Pia ifahamike kuwa michezo ni sehemu ya majukumu ya kila siku kwa mwanajeshi hivyo kupitia michezo hii tunaweza kujenga na kuimarisha utimamu wa mwili na afya ya akili, Kujenga moyo wa kishujaa, ujasiri, ukakamavu na kujiamini, Kubaini, kukuza na kulea vipaji vya Maafisa na Wapiganaji kimichezo.
Aidha kuimarisha mahusiano kati ya Jeshi na Raia/Jamii kupitia michezo hivyo kuendeleza ari ya Jeshi kujitangaza kupitia michezo kutoa burudani kwa wananchi/jamii na hivyo kuepusha jamii na tabia zisizostahili, kujenga ushirikiano, upendo, undugu na uzalendo miongoni mwa wanajeshi na raia.
“Mashindano haya yatahusisha timu za michezo mbalimbali kutoka Kamandi zetu zote za Jeshi ambazo ni Kamandi ya vikosi Chini ya Makao Makuu ya Jeshi, kamandi ya Jeshi la nchi Kavu, kamandi ya Jeshi la Anga ,Kamandi ya Jeshi la wanamaji, Kamandi ya Jeshi la Akiba na Jeshi la Kujenga Taifa.
Ameendelea kusema kuwa Mwaka huu mashindano yatakuwa makubwa zaidi kulinganisha na miaka iliyopita kwani kuna ongezeko la michezo mipya ambayo haikuwahi kuchezwa katika mashindano yaliyopita ambapo Kutakuwa na michezo yenye asili ya kijeshi na michezo ya kimashindano, kwa maana hiyo michezo itakayoshindaniwa jumla yake itakuwa idadi kumi na tatu.
Ikiwemo Mpira wa Miguu, wanaume, Mpira wa Netiboli, wanawake, mpira wa wavu, kwa wanaume  na wanawake, Mpira wa mikono, kwa wanaume na wanawake, Mpira wa kikapu, Wanaume  na Wanawake
Mchezo wa Riadha, Wanaume na Wanawake, Mchezo wa Ngumi, Wanaume na Wanawake
Mchezo wa kulenga Shabaha, Wanaume na Wanawake ambapo michezo mipya iliyoongezeka idadi mitano ambayo ni Mchezo wa Kuogelea, Wanaume na Wanawake, Mchezo wa Kuruka vikwazo, Wanaume na Wanawake ,Mchezo wa Gofu, Wanaume  na Wanawake na  Mchezo wa Mieleka kwa Wanaume na Wanawake, Mchezo wa Vishale (Darts),  kwa wanaume  na Wanawake.
Aidha, kulingana na ongezeko la michezo vitatumika viwanja katika maeneo tofauti ifuatavyo:
Uwanja wa Azam, utatumika kwa ajili ya mechi za football, sherehe za Ufunguzi na ufungaji.
Viwanja vya Kambi ya Jenerali Twalipo – Mgulani, viwanja hivi vitatumika kwa ajili ya michezo ya Mpira wa kikapu, netiboli, mikono na wavu, vile vile michezo ya ngumi, kuruka vikwazo na mieleka ambayo nayo itafanyika Twalipo.
Viwanja vya Gofu Lugalo, utachezwa mchezo wa Gofu.Viwanja cha Msasani beach, mchezo wa vishale (darts).
Kiwanja cha 501 KJ (Lugalo), kitatumika kwa ajili ya mchezo wa mpira wa miguu.
Makao Makuu ya Kamandi ya Wanamaji (Navy,) mchezo wa kuogelea utachezwa.
Katika sherehe za ufunguzi mgeni rasmi atakuwa Mhe Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Mhe. Stergomena Lawrence Tax na Sherehe za Ufungaji mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda na  Sherehe zote zitafanyika katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi.



Prev Post Makalla: Barabara ya Mpwapwa Njiapanda Kongwa Kujengwa Lami
Next Post Airtel UNICEF Waunganisha Shule 30 Mkoani Dodoma Na Intaneti Ya Bure
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook