
• Rais Dkt Samia ametoa fedha mkandarasi ameanza maandalizi
MPWAPWA: KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Cham cha Mapinduzi (CCM)Taifa, CPA Amos Makalla amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Mpwapwa-Kongwa-Mbande ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami.
Makalla ameeleza hayo leo Juni 23, 2025 wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo.
Makalla amesema CCM ndiyo chama chenye dhamana kwa watanzania na katika kuthibitisha hilo Rais Samia ametoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika ambayo imeacha alama kwa kugusa kila sekta.
Akieleza hayo Makalla amesema katika barabara tajwa tayari mkandarasi ameshapewa na yupo katika maandalizi ya utekelezaji wa ujenzi wa barabara hiyo.
“Ukiwasikiliza wabunge na Mkuu wa Wilaya wameeleza miradi mbalimbali iliyotekelezwa, ningemwambia Mbunge wa Kongwa Job Ndugai aseme habari ya Kongwa tungekesha, kila mahali kuna alama ya maendeleo yaliyofanywa na serikali.”
Ameongeza: “Kuna wananchi wameshuhudia shule zikijengea, elimu bila malipo, vituo vya afya, umeme vijijini, madaraja yakijengwa, mambo ni mengi yaliyofanywa na hayo yamesababisha wananchi kwa kauli moja katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kukiamini CCM, yote yamefanywa chini ya Rais Samia,” amesema.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!