Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

CCM: Kina kazi ya kutumikia Wananchi si kutukana matusi majukwaani

  • 40
Scroll Down To Discover

Chama Cha Mapinduzi kimesema viongozi wake wana kazi ya kufanya Siasa Safi na utekelezaji kwa Vitendo kunakotokana na matakwa ya Sera zake na kutumikia wananchi bila kuwabagua.

Vile vile , CCM kimejipambanua kuwa ndio chama pekee Barani Afrika, kinachoheshimu heshima na utu wa kila binadamu.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamisi Mbeto Khamis, ameeleza hayo huku akisema upinzani utaendelea kwa miaka mingi ijayo kupata tabu kushinda na sera za CCM.

Mbeto alisema Siasa ya CCM na sera zake hazibaki ndani ya vitabu, kwenye makabati na katika mabango , bali hutekelezwa kwa vitendo ili kuleta maendeleo yanayoshuhudiwa hivi sasa Vijiji na Mijini.

Alisema kuna Vyama kadhaa Barani Afrika ambavyo ni hodari kwa kutunga Sera na kuandika Ilani za Uchaguzi lakini vinaposhika dola , hushindwa kutimiza wajibu kwa jamii .

“Siasa na Sera za CCM zinakwenda sambamba na utekezaji kwa vitendo ili kuleta msukumo chanya wa maendeleo.Wapinzani wetu ndipo wanapojikuta hawakubaliki kwa Wananchi” Alisema Mbeto

Aidha Mwenezi huyo, alisema siku zote kadri mtu akiitazama Tanzania, aidha Bara au Visiwani , kumekuwa na hatua kubwa za kimaendeleo kutokana na utekelezaji wa Sera za CCM.

” Watendaji wa Chama na serikali za CCM kutwa kucha huchemsha bongo na kufanya mambo yasiende mrama. Kuchanua kwa maendeleo nchini ni uthubutu wa kubeba dhima na dhamana ya utekelezaji wa Sera ” Alieleza

Mbeto alisema kwa sababu hiyo, ndio maana wananchi wanapohudhuria mikutano ya hadhara ya upinzani , huwasikiliza viongozi wao wanavyotoa matusi na jeuri kisha huwapuuza na kuondoka .

“ACT, Chadema, CHAUMA ,NCCR-MAGEUZI , Tadea na vingine magari yao yanapita katika barabara zilizojengwa na Serikali za CCM .Hata wanapoumwa hutubiwa kwenye hospitali zenye ,madaktari, dawa na vifaa tiba bora ” Alisisitiza

Katibu huyo Mwenezi aliongeza kusema ndio maana viongozi wa Upinzani , wanapokuwa majukwani hukwepa kuzungumzia ushindani wa sera ,badala yake hutupa matusi ,kejeli na Siasa za Ubaguzi.



Prev Post Afariki Dunia Akiwa na Mke wa Mtu Katika Guest House Mkoani Njombe – Video
Next Post Msigwa Atoa Onyo Kuhusu Matumizi Mabaya ya Mitandao ya Kijamii – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook