

Erasto Raphaely Kabupa (50) mkazi wa kijiji cha Igelehedza kata ya Ilembula wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe amefariki dunia wakati akishiriki tendo la ndoa na anayedaiwa kuwa mke wa mtu katika nyumba ya kulala wageni (Guest house).
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amethibitisha taarifa za kifo hicho ambapo amesema June 8,2025 majira saa mbili usiku, Erasto (marehemu) alikuwa na mwanamke anayedaiwa kuwa mke wa mtu katika nyuma ya kulala wageni na wakati wakiendelea na tendo alizidiwa ghafla na kukimbizwa kituo cha afya Ilembula lakini alifikishwa akiwa tayari amepoteza maisha.
“Baada ya kufikishwa hospitali alitambulika amefariki dunia lakini awali alifika na mwanamke kwenye gesti inayoitwa Mwendavanu kwa lengo la kushiriki tendo la ndoa na kimsingi sisi hatuna taarifa kama alikuwa ametumia dawa hilo ni swala la kidaktari” amesema Kamanda Banga.
RPC Banga amesema kutokana na aina ya tukio Jeshi la Polisi haliwezi kumkamata mwanamke aliye kuwa pamoja na marehemu huyo kwasababu wanaume wengi pia kwenye ndoa wamekuwa wakipoteza maisha kwasababu hiyo, hivyo hawawezi kumkamata mtu kwa kufanya mauaji kwa tendo hilo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!