
Dar es Salaam, Juni 5, 2025 — Chama cha ACT Wazalendo leo Alhamisi Juni 5, 2025 kimempokea rasmi Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, aliyejiunga na chama hicho kama mwanachama mpya katika hafla iliyofanyika Magomeni, jijini Dar es Salaam.
Sheikh Ponda, ambaye ni miongoni mwa viongozi wa dini ya Kiislamu wanaotambulika kwa ushawishi mkubwa nchini, alitangaza uamuzi wake wa kujiunga na ACT Wazalendo mbele ya umati wa wafuasi na viongozi wa chama hicho, akisema kuwa wakati umefika kwa viongozi wa dini kushiriki kikamilifu katika kupigania haki, usawa na maendeleo ya kweli ya wananchi.
“Nimeamua kujiunga na ACT Wazalendo kwa sababu ninayaona matumaini ya kweli ya mabadiliko ndani ya chama hiki. Tunahitaji siasa zenye maadili, zinazojali watu na zinazoweka mbele maslahi ya umma, si maslahi binafsi ya wachache,” alisema Sheikh Ponda wakati wa tukio hilo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!