Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Uturuki Waanza Mchakato Wa Kuandika Katiba Mpya, Wataalamu Wa Sheria Kuanza Mchakato

  • 19
Scroll Down To Discover

Uturuki Waanza Mchakato wa Kuandika Katiba Mpya Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki ameteua timu ya wataalamu wa sheria kuanza mchakato wa kuandika katiba mpya.

Wakosoaji wake wanasema katiba hiyo itamruhusu kiongozi huyo kusalia madarakani hata baada ya mwaka 2028, pale muhula wake wa sasa utakapomalizika.

Akizungumza na maafisa wa chama chake, Erdogan alisema wataalamu hao kumi aliowachaguwa watatimiza jukumu la kupatikana kwa katiba mpya, kuchukuwa nafasi ya sasa ambayo iliandikwa baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 1980.

Erdogan, ambaye ameitawala Uturuki kama rais tangu mwaka 2014 na aliyekuwa waziri mkuu kwa zaidi ya muongo mmoja kabla ya hapo, amekuwa akiwania upatikanaji wa katiba mpya, akisema kuwa iliyopo sasa imepitwa na wakati na bado inabeba athari za utawala wa kijeshi, licha ya kufanyiwa marekebisho mara kadhaa.



Prev Post Mbunge Shigongo Apongezwa kwa Ubunifu wa Madarasa Janja Kupitia TEHAMA
Next Post Rais Ruto Aomba Radhi Kwa Tanzania Kwa Kinachoendelea – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook