

Serikali kupitia kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zainab Katimba imempongeza Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo kwa kuanzisha madarasa janja (smart classes) ili kukabiliana na uhaba wa walimu katika jimbo hilo.
Katimba ameyasema hayo wakati akijibu swali la Shigongo bungeni jijini Dodoma aliyetaka kujua mpango wa serikali kupeleka walimu wa masomo ya sayansi katika jimbo hilo.
Kupitia madarasa janja, mwalimu aliyepo kituo kimoja anaweza kufundisha kwenye madarasa mengi yaliyopo sehemu tofauti kwa kutumia mifumo ya TEHAMA.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!