Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Waziri Mkuu Kumwakilisha Rais Samia Maonesho ya World Expo 2025 Osaka, Japan

  • 13
Scroll Down To Discover

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 23, 2025 amewasili Osaka nchini Japan kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye maonesho ya kimataifa ya Osaka (World Expo 2025 Osaka).
Akiwa nchini Japan, Mheshimiwa Majaliwa atashiriki katika kongamano la biashara, uwekezaji na utalii ambalo litahusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Japan.
Pia, Waziri Mkuu atashiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.
Maonesho hayo yalianza tangu Aprili 13, 2025 na yanatarajia kumalizika Oktoba 13, 2025, hii ni mara ya pili kwa Japan (Osaka) kuwa mwenyeji wa maonesho haya ya kimataifa, ambapo mara ya mwisho yalifanyika 1970 (EXPO 1970).



Prev Post Wiki ya Asasi za Kiraia (Azaki) 2025 Kufanyika Juni Mount Meru Jijini Arusha
Next Post Simba Yatembelea Na Kuomba Dua Kaburini Kwa Hayati Mwinyi Visiwani Zanzibar
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook