
Simba SC imetembelea kaburi la Hayati Ali Hassan Mwinyi visiwani Zanzibar na kufanya dua maalum ya kumuombea apumzike kwa amani. Pia waliiombea timu hiyo mafanikio, huku ikijiandaa kutafuta ushindi katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Zanzibar, baada ya kupoteza mechi ya kwanza kwa mabao 2-0. Mashabiki wamebaki na matumaini ya kushuhudia Simba ikiibuka mabingwa na kuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!