Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Makalla: Uchaguzi Hauwezi Kusogezwa, CHADEMA Jipangeni 20230

  • 4
Scroll Down To Discover

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema uchaguzi hauwezi kusogezwa  mbele kwani wamejipanga kushiriki uchaguzi na hawawezi kuwa sehemu ya kuvunja katiba, hivyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wajipange 2030.

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla ameeleza hayo leo Mei 15 wakati akizungumza na wananchibwa Jimbo la Kilosa na Mikumi katika Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro akimalizia ziara yake ya siku saba iliyokatishwa kupisha maembolezo ya Mzee Cleopa Msuya.

Makalla amesema hakuna jambo la dharura wala vita la kufanya uchaguzi uhairishwe na wala nchi haipo kwenye vita wala jambo lolote la kutisha kusema uchaguzi ushindwe kufanyika.

Amesema CCM ni chama kinachoheshimu demokrasia na hawapo tayari kuvunja katiba na kwakuwa wenye Chadema hawashiriki uchaguzi wasubiri 2030.

“Wenzetu hawa nimesikia walianza juzi Bukoba, Geita wameenda Mwanza nikasikia Myika na Heche wanasema tunaomba uchaguzi usogezwe mbele mpaka tufanye mabadiliko,” amesema Makalla.

Ameongeza: “hakuna mwenye mamlaka ya kusogeza uchaguzi uchaguzi upo kwa takwa la kikatiba na mimi nawaambia Mnyika na Heche tuko tayari kwa uchaguzi sijui wako wapi, ACT wameanza kuchukua fomu na sisi tumejipanga kwenye chama chetu tunaenda kwenye uchaguzi”.



Prev Post Mwili wa Charles Hilary Ulivyowasili Zanzibar Kwa Mazishi
Next Post Waite Darstate Wakudaie Deni Lako Sehemu Yoyote – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook