
Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasilino Ikulu Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Charles Hilary umewasili Mei 14, 2025 Visiwani Zanzibar na kupokelewa na ndugu,jamaa na Marafiki wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Idrisa Kitwana Mustafa.
Baada ya mapokezi hayo Mwili wa Hayati Charles ulipelekwa nyumbani kwao Makadara na kufanyiwa Ibada Fupi na maombi.
Itakumbukwa kuwa Charles alifariki alfajiri ya tarehe 11 Mei 2025 jijini Dar es salaam katika Hospitali ya Mloganzila na anatarajia kuzikwa kesho katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar saa kumi za jioni.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!