

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema saa 06:45 usiku May 13,2025 katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere lango namba 03 (terminal 03) lilimkamata Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Amani Golugwa, akiwa katika maandalizi ya kusafiri
kuelekea Brussels nchini Ubelgiji.
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam SACP Faustine Mafwele amesema “Jeshi la Polisi lilimkamata Naibu Katibu Mkuu huyo kufuatia taarifa za siri kuwa amekuwa na mienendo ya kuondoka na kurudi nchini bila kufuata taratibu za kisheria hapa nchini”
“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linaendelea na uchunguzi wa kina wa taarifa hizi kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Usalama kuhusu suala hilo, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa Wananchi kuendelea kuwa Watulivu wakati uchunguzi ukiendelea na kupuuza taarifa za upotoshaji kuhusu hatua hizi za kisheria zinazomhusu Mtajwa”
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!