
Kilimanjaro, Mei 13, 2025 — Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro na mikoa ya jirani wamekusanyika leo katika Kanisa la KKKT Kristo Mchungaji Mwema, Dayosisi ya Mwanga, Jimbo la Kaskazini, Usharika wa Usangi Kivindu, kushiriki ibada maalumu ya mazishi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Cleopa David Msuya.
Viongozi wa Serikali, viongozi wa dini, na wawakilishi wa taasisi mbalimbali wamehudhuria ibada hiyo ambayo imefanyika kwa heshima kubwa kwa kiongozi huyo aliyelitumikia Taifa kwa muda mrefu.

Msuya, aliyefariki dunia mapema wiki iliyopita, alikumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kisiasa nchini Tanzania. Katika hotuba zao, viongozi mbalimbali walieleza kuwa alisimama kama kiongozi shupavu, mzalendo na mpenda haki aliyeacha alama isiyofutika katika historia ya Taifa.
Ibada hiyo imeongozwa na Askofu Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini, akisisitiza juu ya umuhimu wa kuenzi amani, mshikamano, na maadili aliyoyaishi Hayati Msuya.
Mazishi yamefanyika katika makaburi ya familia yaliyopo Usangi Kivindu, ambako alizaliwa na kukulia.




Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!